Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amesema kuanzia sasa hataki kusikia changamoto zinazohusiana na Usafiri wa Mabasi yaendayo kasi zikiwemo changamoto za abiria kukaa muda mrefu katika vituo wakisubiri usafiri ambapo amemuagiza mtendaji mkuu wa DART kushirikiana na UDART kuhakikisha mabasi mapya ya mwendo kasi yanafika upesi ili kuondoa kero ya usafiri kwani wananchi wamesubiri kwa muda mrefu.
Mchengerwa ameyasema hayo wakati akizindua Mageti Janja na kadi janja za mfumo wa teknolojia ya kielektoniki ambapo ameagiza kadi hizo kuanza kutumika maramoja kwavile kadi hizo zitaondoa matumizi ya karatasi,zitaondoa msongamano wa foleni na kwamba wasafiri watakuwa hawana haja ya kubeba pesa za nauli mfukoni baada ya kuwa wamenunua kadi kwa shilingi elfu 5 na kuisajili na kuongeza kuwa kadi hizo zitaondoa malalamiko ya wananchi kudai kudhulumiwa chenchi zao pindi wanapolipia ticket.
Amewataka watendaji wa DART na UDART kuwashirikisha wawekezaji wa zawa katika zabuni za uendeshaji wa mabasi badala ya kusubiri wawekezaji kutoka nje ya Nchi.