36 views 54 secs 0 comments

MAJALIWA:SUALA LA KULINDA NCHI NI WAJIBU WA WATANZANIA NA VYOMBO VYA USALAMA

In KITAIFA
August 29, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa suala la kuilinda nchi ni wajibu wa Watanzania wote kwa ushirikiano wa vyombo vya ulinzi na usalama.


Majaliwa amesema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vina jukumu la kupokea taarifa mbalimbali zinazoonyesha uvunjifu wa amani popote pale .

Waziri mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Vitu Maalum,  Mhe.  Anatropia Theonest, aliyetaka kujua mikakati ya Serikali kuhusu matukio ya utekaji yanayoripotiwa kutokea nchini.

Aidha Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita (6) inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan,  imeendelea kujikita kusimamia misingi ya amani katika nchi.

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram