151 views 2 mins 0 comments

MHE KAPINGA SERIKALI IMEDHAMIRIA KILA MTANZANIA KUPATA UMEME

In KITAIFA
August 22, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Lengo ni kuimarisha unganishwaji wa huduma ya umeme katika maeneo yote nchini

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kila mtanzania kupata umeme kwenye nyumba yake kuanzia  ngazi za mikoa mpaka vitongoji.

Mhe. Kapinga amesema hayo Agosti 21, 2024 wakati  wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango kwenye uwekaji jiwe la Msingi Ujenzi wa Daraja la Mto Hurui lililopo katika Kijiji cha Hurui Wilaya ya Kondoa akiwa ziarani mkoani Dodoma.

Daraja hilo limegharimu Kiasi cha shilingi  bilioni 1.6, na litarahisisha shughuli mbalimbali za wananchi ambao hapo awali lilikatika na kusababisha wananchi wa wilaya hiyo na wilaya ya babati mkoani Manyara kukosa mawasiliano kwa muda mrefu.

Kapinga ameeleza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatoa fedha ili kuanzia hatu ya usambazaji umeme katika vitongoji, na vitongoji vya Huruni vipo kwenye mpango huo.

Alisema kuwa, Hatua ya kwanza ya kufikisha umeme vijijini imekamilika na adhma ya serikali ya awamu ya sita ni kuendelea kuboresha maisha ya kiuchumi na kijamii hasa kwenye upatikanaji wa umeme.

Wananchi wa maeneo hayo wamefurahishwa na hatua za ujenzi wa Daraja, kwani hapo awali walikuwa wakipita kwa shida kwenye eneo hiilo  na kukosekana kwa Mawasiliano na kuishukuru Serikali kwa kazi nzuri  ya ujenzi wa daraja Hilo.

Daraja hilo lenye urefu wa  mita thelathini lina uwezo wa kubeba uzito wa hadi tani sabini.

Makamu wa Rais alitembelea pia shule ya Msingi Iboni inayojumuisha watoto wenye mahitaji maalum na kutoa rai kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu kuacha tabia ya kuwaficha na kuwanyima fursa muhimu ya kupata elimu.

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram