54 views 49 secs 0 comments

KAMATI YA BUNGE NA WIZARA YAANDAA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA 50 WA SHIRIKISHO LA WAFUGAJI NYUKI DUNIANI 2027

In KITAIFA
August 22, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ikiongozwa na Mwenyekiti Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) leo Agosti 22,2024 Bungeni jijini Dodoma, imepokea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Maliasili na Utalii ikiwemo taarifa ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 50 wa Shirikisho la Wafugaji Nyuki Duniani (APIMONDIA) utakaofanyika Mwaka 2027.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii (anayeshughulikia Utalii)  Nkoba Mabula pamoja na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram