167 views 2 mins 0 comments

PASS LEASING NI MFANO WA KUIGWA

In KITAIFA
August 04, 2024



Na Richard Mrusha Dodoma

NAIBU Waziri wa Kilimo David Silinde amewaasa wadau wa masuala ya kilimo kuiga mfano wa Pass leasing wa kutoa matrekta  kwa wananchi 9 ambayo yanakwenda kurahisisha kilimo kwa wananchi hao.

Akizungumza katika banda la Agricom ambako zana hizo zilikabidhiwa kwa walengwa wakiwemo wanawake na vijana ambao ndiyo nguvukazinya ya Taifa Silinde amesema ,kama Serikali itaendelea kuwaunga mkono.

“PASS Leasing  tunawashukuru kwa kazi mnayofainya ya kuwawezesha wananchi zana hizi za  kilimo ,na  hili ni jambo ambalo sisi kama serikali tutaendelea kuwasapot na inahitaji wadau kama ninyi kuhakikisha hii sekta ya kilimo tunaipush pamoja .amesema na kuongeza kuwa

“Na siku zote tumekuwa tukizungumza kwamba Sisi kama Wizara hatulimi,wanaolima ni wananchi na kilimo ni sayansi ambayo inahitaji ushirikiano wa pamoja ili kwenda mbele,kwa hiyo kwa kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ana dhamira ya dhati kuhakikisha kwamba kilimo tunakibadilisha kwenye viwango vingine .

Silinde amesema, wizara imekusudia kwamba tuna’change’ tukitazame kilimo kwa mtazamo chanya kwa  kutumia Teknolojia za kisasa ambazo tutarahisisha ulimaji lakini pia tunatransform kilimo chetu badala ya kutegemea mvua tuige na kilimo kinachotegemea maji kwa kujenga mabwawa ya umwagiliaji yatakayowezesha wananchi kulima kwa tija

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya PASS Leasing Rosebard Kurwijila amesema kampuni hiyo itawawezesha wakulima kupata zana zankilimo ili waweze kuzalisha kwa tija.

“Na tunapotoa vifaa hivi tunazingatia mnyororo wa thamani tangu kulima mpaka kuyaandaa mazao ,na mpaka sasa tumeshawawezesha wakulima 1,000.”amesema Kurwijila

Baadhi ya wakulima walizokabidhiwa matrekta hayo  ameishukuru PASS Leasing kwa kuwapatia matrekta hayo ambayo yanakwenda kuwasaidia kuongeza tija kwao na Taifa kwa ujumla.

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram