20 views 32 secs 0 comments

WAZIRI MKUU KUWA MGENI RASMI KATIKA MBIO ZA HISANI ZA MAENDELEO BANK

In MICHEZO
August 03, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio za hisani za Maendelo Bank zenye lengo kukusanya milioni 200 zitakazo saidia vituo viwili vya watoto  kwenye Hospitali ya KCMC Mkoani Kilimanjaro ambapo itasaidia  watoto waliozaliwa chini ya miezi 9 pamoja na kituo cha watoto yatima cha mtoni Dikonia kilichipo Bagamoyo Mkoani Pwani.



Hayo ameyasema Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Bank PLC, Peter Tarimo  Jijini Dar es salaam leo Agust 2,2024 wakati akizindua  mbio hizo zitafanyika tarehe 7.9.2024 kwenye viwanja vya farasi Jijini Dar es salaam

“Katika Hospitali ya KCM zaidi ya watoto 500 wanazaliwa kila mwaka lakini uhitaji ni mkuwa kuliko vifaa vinavyohitajika na kwasababu hiyohiyo watoto wengi wamekuwa wakifariki kwa sababu ya kukosa huduma mbalimbali ikiwemo vitanda na changamoto nyingine” amesema



“Takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 25% mpaka 30 ya watoto wanaofika pale watoto karibu 150 kati ya 500 wanafariki  moja ya sababu kubwa iliyotajwa ni ukosefu wa vifaa”amesema Tarimo



Ameongeza kuwa mbio za mwaka huu zitahusisha m za kilometa 2.5, 5, 10 na kilometa 21 huku tishirt zitaunzwa kwa 35000 pamoja na 150,000 za kitanzania.

Kauli mbiu ya mbio hizo ni hatua ya faraja msimu wa pili.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram