96 views 2 mins 0 comments

MWENYEKITI WA BODI GST ATOA MAELEKEZO KUIMARISHA TAASISI

In KITAIFA
August 02, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Prof. Ikingura aongoza Kikao cha 19 Bodi ya GST

Asisitiza kutangaza bidhaa na huduma zinazotolewa na GST

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeelekezwa kuendelea kuitangaza bidhaa inayoizalisha ya vyungu vya kuyeyushia sampuli za  miamba na udongo wenye madini ya dhahabu (crucibles) ili kuongeza makusanyo ya ndani na kuongeza tija kwa Taasisi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya GST Prof. Justinian Ikingura wakati akiongoza kikao cha 19 cha Bodi ya GST  kilichofanyika Agosti 01, 2024 katika ukumbi wa Prof. Abdulkarim Mruma Jijini Dodoma.

Aidha, Prof. Ikingura ameitaka Taasisi hiyo kuongeza jitihada za kujitangaza hasa katika huduma zitolewazo na maabara ya _geotechnical_ kwa wadau mbalimbali ili kuitumia GST katika utafiti na uchunguzi wa sampuli za miamba na udongo.

Aidha, Prof. Ikingura ameipongeza Menejimenti ya GST kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya na kuitaka Taasisi hiyo kuandaa mpango wa kutoa elimu kwa wadau katika maeneo mbalimbali ikiwemo matumizi ya taarifa za jiosayansi katika utafutaji na uchimbaji wa madini; na ubora wa vyungu vya kuyeyushia sampuli za miamba na udongo wenye madini ya dhahabu kwa lengo kuongeza uelewa kwa watumiaji wa bidhaa hiyo.

Naye, Kaimu Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Maabara ya GST Notka Banteze amesema Menejimenti ya GST imepokea maelekezo ya Bodi hiyo na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa.

Pia, ameishukuru Bodi hiyo kwa ushauri na maelekezo waliyoyatoa ambapo ameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Bodi hiyo.

Kikao hicho cha 19 cha Bodi ya GST kimelenga kujadili taarifa ya utekelezaji ya GST ya kipindi kinachoanzia Aprili hadi Julai 2024.

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram