
Na Madina Mohammed PWANI RUFIJI

Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Rufiji imewashukuru TMDA Kwa kuwapatia msaada wa dawa na dawa hizo kusambazwa Katika zahanati zilizopo katika Halmashauri ya utete Ili wananchi wapate huduma za dawa bila ya kusita
Amesema Tunawashukuru uongozi wa TMDA Kwa kuona umuhimu wa kutuletea dawa kama Wilaya,sisi kama Wilaya tunalojukumu Kwa kuhudumia au kutoa huduma na tiba Kwa wananchi
Ameyasema hayo 1 August 2024 Mkuu wa Wilaya Meja Edward Gowele wakati wakizungumza na Mwandishi wa habari Amesema Dawa hizi ambazo zilizotolewa siku ya Leo na TMDA zitakwenda kuwa dawa muhimu Kwa watu Wetu na zenye faida

“Tunaahidi kwamba Kwa niaba ya uongozi wa Wilaya kwamba sisi tunaendelea kushirikiana na TMDA lakini pia tunaahidi dawa hizi zinakwenda kutumika vilivyo na kutakuwa na utaratibu mzuri wa kutawanyisha dawa hizi Kwa zahanati zetu Ili wananchi Wetu waweze kupata matibabu bila kusimama”Amesema Gowele
Nae mganga mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya Rufiji khamis Abdallah Amesema Tunawashukuru TMDA Kwa kutupatia bidhaa hizi za Afya,kimsingi tunauhitaji Katika familia zetu ukizingatia Katika mwaka huu mpya wa 2024/2025 tunanafasi mbili tunaenda kufungua ambazo kimsingi zitaitaji sana hizi bidhaa za Afya Kwa ajili ya kwenda kuanzisha huduma,

“dawa hizi kutoka TMDA zimekuja Muda muafaka ambazo kimsingi zitatusaidia kwenda kuanzisha huduma Kwa zile zahanati mpya ambazo tutazoenda kuzizindua Katika mwaka huu wa fedha 2024/2025 zitasaidia kuleta mulali Kwa watumishi Kwa kufanya kazi pindi unapokuwa na bidhaa za Afya kunamsaidia hata kutoa matibabu Bora Kwa wananchi”Amesema Abdallah
Aidha Meneja wa mamlaka ya dawa na vifaa Tiba TMDA Kanda ya mashariki Adonis Bitegeko Amesema TMDA Kwa majukumu yake ya msingi Katika mwaka uliopita wa fedha 2023/2024 iliweza kubaini na kukamata dawa na bidhaa mbalimbali ambazo zilionekana zipo Katika maeneo ambayo hayaruhusiwi

Amesema dawa hizi na vifaa Tiba zinathamani ya shilling milioni ishirini na Moja laki Saba na elfu kumi na tano na mia hamsini za fedha za kitanzania TMDA imefanya huwakiki wa dawa hizo na kuona kwamba zinafaa Katika matumizi na baada ya kuziteketeza tumeona kwamba umuhimu wa kuzigawa Katika Wilaya ya Rufiji na Katika ugawaji huo tumeangalia kwenye maeneo ya uwitaji maana maeneo ya uwitaji yapo mengi tukaona kwamba Wilaya ya Rufiji kama munavyoifahamu ilipata changamoto ya athari za mafuriko Katika Mvua kubwa

“Lakini pia Kuna vituo vipya vya afya vinajengwa zahanati kama alivyosema mganga mkuu wa Wilaya kuwa Kuna vituo viwili vinajengwa kwani zinauwitaji wa dawa na vifaa Tiba”Amesema Bitegeko
Hata hivyo Tulibaini tukaona haja ya kuja kusaidia na kuleta bidhaa huku Kwa ajili ya matumizi na kimsingi ni bidhaa zilizopo ni Bora na salama na kwamba tumezihakiki na tumeona zitasaidia na tumeimalisha huduma za Afya Katika Wilaya ya Rufiji

Aidha Amesema Tunatoa Rai Kwa halmashauri zote zile ambazo tunashirikiana nazo Kwa udhibiti wa dawa na vifaa Tiba ni kwamba tunaweka mkazo Katika kudhibiti Katika dawa na vifaa Tiba ilikuona kwamba kila kinachotumika Katika maeneo yetu kikobora na salama na sisi TMDA tunawaasa wafanyabiashara wanaotoa huduma wanapaswa kuzingatia Sheria kuona kwamba dawa na vifaa Tiba ni vile ambavyo unazoruhusiwa kuwa navyo na kusambaza wale wa jumla wanapoouza dawa kwenye maduka ya rejareja wanaitajika wauze.katika maduka muhimu ambazo wanapaswa wawenazo ambazo zimesajiliwa na wauze dawa zinazoitajika na wasiuze dawa za serikali

Tuendelee kupata ushirikiano Kwa pamoja na tuendelee kushirikiana sisi kama taasisi ya wizara ya afya tunajukumu la kuchangia na kuona kwamba tunalinda afya za wananchi