
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Imeelezwa kuwa Serikali imelenga kupata faida katika huduma ya usafiri wa treni za umeme za Mwendokasi kupitia usafirishaji wa mizigo na sio kupitia abiria wa kawaida.
Hayo yamesemwa julai 30,2024 na Waziri wa Uchukuzi profesa Makame Mbalawa wakazi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kubainisha kuwa treni za SGR zinauwezo wa kubeba tani elfu 10 za mizigo Sawa na maroli 500 kwa wakati mmoja hali itakayopelekea kupunguza msongamano wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam,kuimarisha fedha yetu na kuongeza soko la ndani.
“Lengo la serikali kujenga Reli ambayo ukiangalia ndani ya Nchi za Afrika sisi Tanzania ndio nchi pekee yenye mtandao mkubwa wa reli ya kisasa yenye Km 720 na kupitia reli hii Mizigo ndiyo itakayoleta faida kubwa na sio wasafiri wa kawaida,mpaka sasa serikali imetumia Dolla milioni 3.138 kukamilisha ujenzi wa reli huku Shilingi Trillion 1.3 zimetumika kununua vitendea kazi vikiwemo mabehewa 89, seti 10 za vichwa vya treni ya mchongoko na vichwa 19 vya treni ya umeme”.Amesema Profesa Makame Mbalawa.
Aidha ameongeza kuwa uzinduzi rasmi wa treni za SGR utafanyika 1,August jijini Dodoma ambapo Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi.