
Na Anton Kiteteri WAMACHINGA DAR ES SALAAM
Wakati aliyekuwa msemaji wa mabingwa wa soka nchini na mabingwa wapya wa kombe la Toyota Yanga ,ndugu Ally Kamwe kutangaza kujiuzuru nafasi hiyo hapo jana ,rais wa timu hiyo Mhandisi Said Hersi amesema taarifa hizo hazitambui.
“Sina taarifa za Alli Kamwe kuachia ngazi,nilichoelewa ni kwamba inaonekana alikuwa anacheza muziki na alielezea namna ya alivyoondoka stejini” Eng. Heris Saidi rais wa Yanga akizungumza wakati akiwa katika kipindi Sports Arena cha Wasafi FM.
Taarifa za Ally Kamwe kujiondoa kwenye nafasi hiyo zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii mara tu baada ya mechi ya kombe la Toyota kuhitimishwa katika ya Young Africa na Kaiser Chief ambapo Yanga waliibuka mabingwa Kwa kuwachapa Kaizer Chief goli 4-0.
Kamwe aliandika “ A Good dancer must know when to Leave a Stage.
𝑀𝑡𝑢𝑚𝑏𝑢𝑖𝑧𝑎𝑗𝑖 𝑚𝑧𝑢𝑟𝑖 𝑎𝑛𝑎𝑡𝑎𝑘𝑖𝑤𝑎 𝑘𝑢𝑗𝑢𝑎 𝑛𝑖 𝑤𝑎𝑘𝑎𝑡𝑖 𝑔𝑎𝑛𝑖 𝑤𝑎 𝑘𝑢𝑜𝑛𝑑𝑜𝑘a 𝐽𝑢𝑘𝑤𝑎𝑎𝑛𝑖.
Maneno ya hekima kutoka katika kinywa cha Patrick Loch Otieno Lumumba;
“Na ni Hekima hii, inanituma mbele yenu Wananchi, Mashabiki na Wanachama wa Klabu yetu pendwa, kuwaambia kuwa, Ni wakati sasa wa kijana wenu kuondoka Jukwaani”,alisema Kamwe.
“Nimesimama Miaka miwili juu ya hili Jukwaa, Tumeimba, Tumecheza, Tumefurahi na Alhamdulillah Tumeshinda pamoja kila pambano Lililokuja mbele yetu”,Aliongea zaidi Kamwe.
“Muda wangu umemalizika na Asanteni sana”,Alihitimisha Kamwe.
Mpaka tunakwenda mitamboni tayari Ally Kamwe amerudishwa kwenye nafasi yake na kupewa mkataba wa miaka miwili kama Afisa habari wa timu.