
Na Rachel Tungaraza
Israel-Golan
Baraza la Usalama wa Taifa la Israel limeidhinisha serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuchukua hatua kali kujibu shambulizi la roketi lililotokea katika Milima ya Golan na kusababisha vifo vya vijana na pamoja na watoto Uamuzi huo umekuja baada ya kikao cha dharura kilichofanyika kufuatia shambulizi hilo ambalo limeacha taifa katika majonzi makubwa.
Waziri Mkuu Netanyahu ameahidi kuchukua hatua kali dhidi ya wale waliohusika na shambulizi hilo, akisema kuwa Israel haitavumilia vitendo vya kigaidi vinavyolenga raia wake.
“Hatutakaa kimya wakati watoto wetu wanauwawa na magaidi. Tutawapata na kuwawajibisha waliofanya uhalifu huu,” alisema Netanyahu.
Shambulizi hilo limeibua hisia kali miongoni mwa Waisraeli kwasababu limepunguza nguvu kazi ya taarifa kwa kwango kikubwa sana, huku wengi wakitaka serikali ichukue hatua madhubuti kuzuia mashambulizi ya aina hii kutokea tena. Baraza la Usalama wa Taifa limesema litaendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa Israel inabaki salama na kwamba haki inatendeka kwa wahanga wa shambulizi hili.
Jumuiya ya kimataifa imelaani vikali shambulizi hilo na kutoa wito wa utulivu huku ikihimiza pande zote kutafuta suluhu ya kudumu kwa mzozo wa eneo la Golan. Umoja wa Mataifa, kupitia msemaji wake, umeelezea kusikitishwa kwake na tukio hili na kutoa wito kwa viongozi wa eneo hilo kushirikiana katika kuleta amani na utulivu.
Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaonya kuwa hatua zozote za kijeshi zinazoweza kuchukuliwa na Israel zinaweza kuongeza mvutano katika eneo hilo ambalo tayari lina hali tete. Wakati huo huo, jeshi la Israel (IDF) limewekwa katika hali ya tahadhari na limeimarisha ulinzi katika maeneo yanayokaribiana na mpaka wa Syria.
Kwa sasa, macho yote yameelekezwa kwa serikali ya Netanyahu kuona ni hatua gani itachukua katika siku zijazo kujibu shambulizi hili na kuhakikisha usalama wa raia wake.