48 views 3 mins 0 comments

BATA BATANI,NCHI KARIBIA 3 KUKUTANA KAZIMZUMBWI

In KITAIFA
July 29, 2024

Na Madina Mohammed KISARAWE WAMACHINGA

Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani imeandaa Tamasha la kimataifa la kihistoria la BATA MSITUNI(Msituni Festival) litakalo shirikisha nchi 3,Tanzania,Uganda na Afrika kusini lenye Lengo la kuhamasisha utalii na kutangaza kituo cha utalii cha Kazimzumbwi kilichopo Pugu Mkoani humo.

Ameyasema hayo Leo Tarehe 29 Julai 2024 Mkuu wa Wilaya ya kisarawe Petro Magoti wakati akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali katika hifadhi ya msitu wa Mazingira asilia,Pugu,Kazimzumbwi uliopo Kisarawe,Pwani ambao unasimamiwa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ambao  upo takribani kilomita 5 Kutoka Gongo la Mboto,Dar Es Salaam.

DC Magoti ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kisarawe amesema tamasha Hilo kwa mwaka huu litakuwa ni la kipekee kwani watanzania watapata fursa ya kukaa katika msitu huo kwa takribani siku sita wakifurahia maisha na mandhari ya msitu huo wenye maeneo mbalimbali ya kuvutia ikiwemo,panzi mwenye rangi ya bendera ya Taifa, ushoroba na Bwawa la Minaki ambapo watapata fursa ya kuvua samaki,kutembea na mitumbwi ndani ya bwawa hilo,kuweka kempu maalum,kula na kunywa na kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya na ngoma za asili kwa siku sita mfululizo kuanzia Septemba 3 hadi 8,2024




“Maandalizi kabambe ya Tamasha hilo yanaendelea na Tamasha hilo ni la kihistoria litafanyika Katika misitu wa kazimzumbi Ambapo burudani mbalimbali zitafanyika zikiwemo Ngoma za jadi za ASILI ya kabila la kizaramo, mashindano ya mbio za mitumbi,mbio za baiskeli na pikipiki pamoja na live band Ambapo wasanii kutoka Uganda,Afrika Kusini na Tanzania Wataburudisha”Amesema Dc Magoti

Aidha Dc Magoti Amesema kuwa serikali imetupa Sehemu yenye fursa na ni lazima tuitangaze, na Tunaeneo zaidi ya Ekari elfu tatu(3000) na tunahitaji kuweka hotel,Migahawa N.k

DC magoti ametoa wito kwa wafanya biashara kujitokeza na kujisajiri ili kupata fursa ya kufanya biashara katika msitu huo,Aidha ameeleza kuwa Tamasha la Msituni festival litakalo fanyika kwa siku 7 kuanzia septemba 3 mpaka septemba 9,2024 limelenga kufungua fursa mbalimbali sanjari na kuifanya wilaya hiyo kuwa ya mfano

Kwa upande wake Afisa Mhifadhi wa wilaya ya Kisarawe kutoka wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS)ambaye pia NI Meneja  wa hifadhi hiyo ya msitu wa asili,Pugu-Kazimzumbwi Baraka Mtemwa amewakaribisha Watanzania kutembelea hifadhi hiyo kwani watajionea vitu mbalimbali ikiwemo miti,ndege panzi mwenye rangi za bendera ya Taifa la Tanzani,Ushoroba na Bwawa la Minaki,huku akisisitiza pia huduma ya malazi kwenye mazingira ya msitu huo pia inapatika na wamejipanga vyema kuwahudumia watakaoshiriki Bata msituni Festival

Tamasha la ‘Bata Msituni Festival’ ni sherehe ya kipekee ya Kiafrika inayolenga kuenzi na kukuza utalii wa mazingira na utamaduni, uzuri wa asili wa Afrika na Tanzania kwa ujumla, na watu wake kupitia utamaduni, sanaa na shughuli mbalimbali za burudani

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram