74 views 30 secs 0 comments

NCHIMBI AWASILI MTWARA

In KITAIFA
July 28, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA ,

KATIBU  Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo amewasili Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku  tano  huku akiwataka wanachama wa CCM kuwa madhubuti kushikamana, kupendana,kushirikiana na kutambua kuwa  wanawajibu wa kuwatumikia watanzania kwa nguvu zote.

Hayo ameyasema leo baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Masasi,amesema wao wanaamini umoja na utulivu unategemewa  sana na  Chama hicho  katika kuwa madhubuti.

Amesema wanaccm  wanawajibu wa kupata viongozi wazuri ambao  wanamoyo wa kuwatumikia wananchi..”wale wazuri miongoni mwetu wapewe nafasi ya kuongoza kwenye jamii.


“Wanaccm wanajukumu la pekee la kuchujana kuhakikisha wanapata viongozi wazuri ambao wanapata nafasi ya kuongoza jamii ambao  tunategemea tukiwapa heshima hiyo wataleta heshima ya CCM na nchi yetu ,”amesema

Dkt.Nchimbi amefurahishwa na umoja waliouonyesha wanaccm wa Masasi kwa namna walivyojitokeza kwa wingi katika mapokezi.

Katika ziara hiyo Katibu  Mkuu wa CCM ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa-NEC, Oganaizesheni, Issa Usi Haji Gavu, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA- Amos Makalla na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa-SUKI-  Rabia Hamid Abdalla.

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram