Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Shirika la reli Tanzania (TRC) Leo hii imeanza Kutoa huduma za safari kutoka dar es salaam kuelekea mjini dodoma ambapo shirika hilo limesema kuwa utekelezaji huo umetokana na juhudi za Mhe Rais Samia suluhu Hassan Ambapo alitoa maelekezo kuwa ifikapo julai mwaka huu 2024 TRC iwe imeshatekeleza mradi wake wa kutoa huduma ya usafiri Kwa wananchi Kwa kuelekea mkoani Dodoma.
Ameyasema hayo Leo Tarehe 25,Julai 2024 Mkurugenzi wa shirika la Reli nchini Tanzania Masanja Kadogosa amesema kuwa kutoka Dar es salaam kuelekea mkoani Dodoma usafiri huo unaenda kurahisisha baadhi ya wasafiri ambao wanatoka sehemu mbalimbali kupitia maeneo ya dar esalaam kuelekea mkoani humo.
Amesema kama shirika wanamshukuru Mungu kwa kukamilisha jambo hilo Kwa wananchi ambao walikuwa wanalisubiria Kwa shauku kubwa.
“Tuna viongozi. Mbalimbali kwenye treni hii ya leo ambayo inaanza rasmi safari za Dar es salaam kuelekea dodoma pia siku za hivi karibuni tutatoa taarifa rasmi ya uzinduzi wa treni hiyo huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Dkt samia suluhu hassani”. Amesema Kadogosa
Aidha Mkurugenzi. Kadogosa. Aliongeza kuwa treni hii inaweza Kubeba mabehewa zaidi ya 14 hadi 20 huku mabehewa hayo yakiwa yamebeba abiria Takribani ya 900. Vilevile baadhi ya Abiria wamekosa tiketi za kuondoka Dodoma hivyo tumeona muamko Mkubwa wa wananchi na kuweza kufurahia usafiri huo wa haraka ambao unatumia muda mchache wa kutoka. ” Amesema mkurugenzi kadogosa”.
Kadogosa Ameongeza kuwa Treni Zetu zipo aina mbili tofauti. Ambazo ni daraja la juu na kawaida kupitia bei elekezi. Ya Mamlaka ya usafiri wa Ardhini ( Latra). Kiwango cha fedha cha kawaida ni elfu thelathini na moja kutoka dar esalaam kuelekea dodoma huku nauli za Kutoka mkoani dar es salaam mpaka Morogoro ni 13000.
Kwa. Upande. Wake Abiria kutoka. Dar es salaam kuelekea mkoani dodoma. Rose mchau. Amesema kuwa leo nina furaha kubwa ya kupanda. Treni.hii ya mwendokasi kwani wameturahisishia katika kutumia muda mchache wa safari ikiwa na tofauti na Magari ya kawaida.
Vilevile Rose ameongeza. Kuwa. Mimi ni mkazi wa dodoma hivyo nilivoona treni hii imekamilika. Pia nawashauri wananchi wote wafike kupanda treni hii kwani ni nzuri. Pia Ina mazingira. Wezeshi kwa watu wa rika zote na mahitaji maalumu pia ni matumaini yangu kuwa katika safari yetu hii tutafika salama