Na Mwandishi wetu WAMACHINGA
Awataka kujindikisha na kujiandaa kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kuchagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwenye uchaguzi mwaka huu ambao watakuwa mstari wa mbele kuleta maendeleo na kutatua changamoto zao kwa haraka.
Dkt. Biteko ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara kijiji cha Lyambamgongo wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
โMuda utakapofika tuwe tayari kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ili tuweze kuchagua viongozi wazuri wenye sifa za kuchaguliwa ambao watasaidia kuleta maendeleo, tunataka jimbo la Bukombe libadilike kwa kuwa na watu wenye maono au mawazo mazuri yatakayosaidia utatuzi wa changamoto zinazotukabiliโ, amefafanua na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.