121 views 2 mins 0 comments

UVCCM YAPOKEA VIFAA VYA KILIMO VYENYE THAMANI YA TAKRIBANI MILIONI 200

In KITAIFA
July 19, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umekabishiwa vifaa vya kilimo na Kampuni ya Kichina ya AMEC Group.

Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano hayo leo Julai 19, 2024 jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohammed Kawaida amesema vifaa hivyo lengo ni kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi pasipo kujali vyama vyao.

Amesema kuwa hadi wanavipata vifaa hivyo, ni kwamba waliituma Kamati ya Utekelezaji ya Vijana Taifa kwenda China kuona ni namna gani wanaweza kuwatafutia fursa vijana ambapo walimtuma Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Jokate Mwegelo.

Kawaida pia amesema wamepata wadau Chuo cha Sayansi cha China ambacho kitawekeza Nchini kwenye ujenzi wa maabara kubwa ya kisasa.

Kwamba Uwekezaji huo ukikamilika utakuwa ni Moja ya Uwekezaji makubwa kufanya na Jumuiya ya UVCCM.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Mwegelo, ameeleza kuwa vifaa hivyo vinagharimu zaidi ya shilingi milioni 200.

Ametaja vifaa hivyo kuwa ni Power Tiller 24 na mashine za kukobolea mpunga (Rice Meal 18) na kwamba juhudi hizi wanafanya ikiwa ni kuunga mkono maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kawekeza kwenye kilimo kama BBT.

Nae mkurugenzi wa kampuni ya Amec Hon.Jason Xiong Jun Amesema Umoja wa Tanzania na china ulikuwa Kwa Muda mrefu haikuwa na tofauti Katika mataifa haya mawili,China company ambayo inayohusikaa na maswala ya kilimo Kwa miaka 40 na imejiimalisha Katika uzalishaji kwenye kilimo kutoka Tanzania

Aidha Nae Mwenyekiti wa chuo Cha Changzhou Building Science Institute CBS Hon.Yang Jiangjin Moja ya kampuni kubwa sana ya china inayofanya biashara,wamekuja kuwekeza hapa Kwa ajili ya kuisaidia Tanzania Katika usafirishaji Bidhaa mbalimbali kwenda nje ya nchi

“Tumekuja kufanya utafiti wa sayansi kutakuwa Katika mikoa ya Kanda ya mashariki Kwa hiyo itawasaidia mainjinia waliopo Tanzania hapa ambao wanaosoma maswala ya sayansi itakuja kutatua matatizo ya wanatanzania na wana matumaini Tanzania na china itakuwa na ushirikiano mzuri”.Amesema Jiangjin

/ Published posts: 1486

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram