78 views 3 mins 0 comments

FCC WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WAFANYABIASHARA KUDHIBITI BIDHAA BANDIA NCHINI

In BIASHARA
July 18, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Waziri mkuu wawataka Wamiliki  wa nembo nchini  kuhakikisha wanafuatilia bidhaa zao sokoni Kwa kutoa taarifa Katika tume ya ushindani FCC pale wanapobaini uwepo wa bidhaa zao wanapoziagiza nchini na wanapoeka alama za bidhaa zao (NEMBO) na kuhakikisha wanadhibiti  bidhaa bandia haziingii nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 18,2024 Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe Exaud Kigahe wakati akimwakilisha   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika Kongamano la maadhimisho ya kuthibiti bidhaa bandia Duniani.



Amesema kuwa wakala wa ushuru wa forodha wahakikishe kuwa wanakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanashirikiana na fcc katika kudhibiti bidhaa bandia kuto kuingia nchini.

“Sheria hii inakataza kuingiza, kutengeneza, kuuza na kuhifadhi bidhaa bandia ambapo adhabu yake ni kifungo  au kulipa faini kama ambavyo imelezwa kwenye sheria hii”na kigahe Ameongeza kuwa

“Wamiliki wanapaswa kutoa elimu kwa umma kuhusiana na bidhaa Zao na hii elimu itawasaidia walaji kutofautisha bidhaa halisi na  zile bidhaa feki na kusaidia walaji kununua  bidhaa halisi” amesema Kigahe

Hata hivyo Kigahe Amewataka wadhalishaji na wafanyabishara nchini kuhakikisha wanapofanya biashara zao zinakidhi sheria ya alama za bidhaa ya mwaka 1993 inayosimamia udhibiti wa bidhaa bandia.



Halikadhalika Kigahe Amesema Udhibiti wa bidhaa bandia si wajibu wa mtu mmoja bali zinahitajika juhudi za pamoja katika kuhakikisha kuwa wanalinda masoko yao na hivyo kuvutia wawekezaji ambao watakuwa na imani na bidhaa zao zinazozalishwa ndizo zinakuwa sokoni.

“Kwa kushirikiana na Fcc na wadau wengine tutahakikisha udhibiti wa bidhaa bandia unakuwa na mafanikio zaidi hasa katika maeneo ya ushirikiano wa kupata mafunzo na nyenzo za kisasa za kutambua na kuthibiti bidhaa bandia”Ameongeza Kigahe

Aidha Kigahe ameiomba Fcc kushirikiana na  wamiliki wa nembo na mamlaka nyingine za serikali katika kuimarisha udhibiti wa biashara haramu za bidhaa bandia na kuhakikisha kuwa wawekezaji wanakuwa na imani ya kuwekeza nchini.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya ushindani FCC William Erio alisema kuwa licha ya elimu kutolewa kwa wananchi juu ya utambuzi wa bidhaa bandia bado kuna haja ya kuendelea kuzungumza na wafanyabiashara umuhimu wa kuweka alama au nembo katika bidhaa zao huku Ummy Mohamed Rajab kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa ZFCC amesema athari za matumizi ya bidhaa bandia hazilengi kudumaza uchumi wa nchi pekee bali hata kwa watumiaji.

Aidha alizitaja shughuli mbalimbali zilizofanyika tangu kuanza kwa maadhimisho hayo hadi kilele chake ambazo ni pamoja na utoaji elimu wa kuacha matumizi ya bidhaa bandia kupitia vyombo vya habari, kufanya moanesho ya wamiliki bidhaa katika ukumbi wa mlimani city Jijini Dar es salaam.

Nae Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Dar es salaam,  salma Maghimbi amesema mahakama itaendelea kutimizia jukumu muhimu katika kutafsiri sheria na kanuni na kuhakikisha kwamba wahalifu  wa bidhaa bandia wanawajibishwa ipasavyo mbele ya sheria.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram