
Na Mwandishi wetu WAMACHINGA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 17, 2024 ametembelewa na ugeni ofisini kwake kutoka Jeshi la Ukombozi la watu wa China ukiongozwa na BRIG GEN CE MWANZIVA Mkurugenzi wa Huduma za Afya TPDF Makao Makuu Dodoma.

RC Chalamila baada ya kupokea ugeni huo amefanya mazungumzo nao, pamoja na mambo mengine waliyozungumza alieleza fursa mbalimbali zilizoko katika Mkoa na Tanzania kwa ujmla kama vile utalii wa hifadhi za mbuga za wanyama,milima na bahari.

Aidha ugeni huo ni miongoni mwa timu ya madaktari wa Jeshi la ukombozi la watu wa China kwa kushirikiana na JWTZ ambao wameweka kambi katika Bandari ya Dar es salaam kuanzia Julai 16,2024 hadi Julai 23,2024 wakitoa huduma za kibingwa za kitabibu kwa wakazi wa Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla.


