58 views 2 mins 0 comments

KLABU YA YANGA YAOMBA KESI IPELEKWE MBELE KWA UCHUNGUZI ZAIDI

In MICHEZO
July 17, 2024

Na Mwandishi wetu WAMACHINGA

“Mnamo tarehe 6/11/2022 watu wawili waliojiita Wanachama wa Young Africans SC walifungua kesi Mahakama ya Kisutu, Bwana. Juma Ally pamoja na Geofrey Mwipopo. Walifungua kesi dhidi ya Wajumbe wa Baraza la Wadhamini ambao ni Mama yetu Fatma Karume, Abeid Mohamed Abeid na Mzee Jabir Katundu kwa madai ya kuwa hawalitambui baraza la wadhamini la Klabu ya Young Africans SC, wakidai liliingia kwa mujibu wa Katiba ya 2010(ambayo wanadai haijasajiliwa)” Simon Patrick

– Mkurugenzi wa Sheria wa Young Africans SC “Klabu tumegundua kuwa, Abedi Mohamed Abedi aligushi sahihi za Mama Fatma Karume, alighushi sahihi Jabir Katundu ambaye alilazimishwa na sahihi ya Mzee Mkuchika. Mzee Jabir Katundu alituma barua yake Kisutu akieleza kuwa hakuwahi kusaini chochote kinachohusiana na kesi hiyo.

Klabu imeomba Mahakama iongeze muda wa Klabu kufanya mapitio ya kesi kwani Klabu haikuwahi kushiriki kwenye kesi hiyo. Klabu vile vile itaomba mahakama ifuatilie jinai ambazo zimeonekana kwenye kesi hiyo ikiwemo kughushi sahihi za baadhi ya Viongozi waandamizi wa Young Africans SC” Simon Patrick – Mkurugenzi wa Sheria

“Kutokana na kutoitambua katiba ya 2010, wanadai wanachama wote si halali, hivyo na Viongozi wote na uanachama wao ambao wanauita wa Katiba ya 2010 ni batili, kwa maana Rais wa Klabu, Makamu wake, Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Viongozi wote walioajiriwa kwa kigezo cha uanachama ni batili pamoja na kazi zote zilizofanywa na Viongozi wote waliopo madarakani nazo ni batili na wanataka ripoti ya fedha na matumizi wakabidhiwe” Simon Patrick – Mkurugenzi wa Sheria wa Young Africans SC

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram