76 views 2 mins 0 comments

MTWARA IMEPATA UWEKEZAJI MPYA WA UCHIMBAJI WA GESI ASILIA WENYE FUTI MILIONI 100

In KITAIFA
July 14, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

KUTOKANA NA Sera nzuri za Uwekezaji zilizowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita, Mkoa wa Mtwara umepata mwekezaji mpya wa uchimbaji wa gesi asilia atakayezalisha futi za ujazo milioni 100 kwa siku.

Hayo yamebainishwa  Julai 11, 2024 na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Halfani Halfani, wakati akizungumza kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema, maeneo ya Songosongo Kilwa na Mnazibay Lindi pia wanazalisha futi za ujazo milioni 250 kwa siku na kiasi kikubwa kinatumiwa kuzalisha umeme.

“Asilimia 50 ye gesi hii inazalishia umeme na kiasi kingine kinatumika kwenye matumizi mengine,” amesema Halfani.


Ameongeza kuwa, Mamlaka hiyo itahakikisha inaongeza wawekezaji kwenye maeneo ambayo yako wazi kwa lengo la kuongeza matumizi ya gesi asilia viwandani na majumbani .


Ameweka wazi kuwa kwa kipindi kirefu wamekuwa hawana wawekezaji wa kutosha hivyo watahakikisha wanaongeza wawekezaji katika maeneo ambayo yapo wazi ili kuleta tija stahiki.


Akizungumzia  majukumu ni kumshauri Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Petroli kuhusu mambo yanayohusu mkondo wa juu wa Petroli nchini.

“PURA tunajukumu la kusimamia shughuli zote za mradi wa kusindika gesi asilia kuwa kimiminika kwa ajili ya soko la nje ya nchi,”amesema.

Halfani ametaja mafanikio yaliyopatikana kwenye gesi asilia kuwa yanachangia kwa wastani wa asilimia 50 ya umeme unaozalishwa nchini, kuongeza matumizi ya gesi asilia viwandani, kupikia majumbani na kwenye magari.

“Kuanzishwa Kwa kanzidata ya watoa huduma wa kitanzania ambapo kampuni za watu zaidi ya watu 2000 wamesajiliwa,”amesema.

Akizungumzia maonesho ya Sabasaba 2024, Halfani amesema hapo zamani maonesho hayo yalikuwa kama gulio ila kwa sasa yameboreshwa na kuwa na hadhi .

“Naipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa kusimamia na kuyawezesha na kuwa na hadhi ya kimataifa,” amesema.

Hata hivyo Halfani wataka wawekezaji wenye uwezo kuwekeza nchini wafike kwa sababu Tanzania ni sehemu salama ya biashara na uwekezaji.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram