71 views 2 mins 0 comments

NAIBU WAZIRI UCHUKUZI ARIDHISHWA NA MASI UJENZI UWANJA WA NDEGE MSALATO

In KITAIFA
July 12, 2024

Na Mwandishi wetu WAMACHINGA

Naibu waziri wa viwanda na Uchukuzi David Kihenzile akilelekea kukagua ujenzi wa uwanja.wa ndege wa kimataifa wa msalato mkoani Dodoma


Naibu waziri wizara ya Uchukuzi David Kihenzile ameeleza kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato mkoani Dodoma ambao umefikia asilimia 67.6 kwa upande wa miundombinu ya njia ya kurukia ndege huku ukiwa umefikia asilimia 32.21 kwa upande wa jengo la abiria.


Naibu Waziri Kihenzile amesema ameridhishwa kwa kujengwa kwa njia ya kurukia ndege yenye urefu wa Kilometa 3 na mita 600 pamoja na eneo litakalokuwa na uwezo wa kuegesha ndege kubwa 13 kwa wakati mmoja lenye urefu wa mita 480.


โ€œNimeshuhudia maendeleo mazuri ya ujenzi wa jengo la zima moto, Jengo la hali ya hewa pamoja na mnara wa kuongozea ndege kimsingi uwanja huu utakapokamilika utakuwa wenye tija kubwa hususani katika Nyanja ya utalii,โ€ Ameongeza Naibu Waziri kihenzile.


Aidha Naibu Waziri Kihenzile ameuppongeza Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege (TAA) kuendelea kufanya kazi nzuri katika kusimamia ujenzi huo ambao unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2025.


Kwa upande wake Meneja Msaidizi Tanroads Mkoa wa Dodoma Mhandisi Elisony Mweladzi amesema jumla ya wananchi 608 wamepata ajira katika mradi wa ujenzi wa njia ya kurukia ndege huku wananchi 947 wakipata ajira katika mradi wa ujenzi wa jengo la abiria huku wageni walioajiriwa ni 31 kwa kila mradi.


Pia Mweladzi amesema kuwa mradi wa njia ya kurukia ndege unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 165.6 huku ule wa ujenzi wa jingo la abiria ukigharimu kiasi cha shilingi bilioni 194.4 huku miradi yote ikitarajiwa kukamilika ndani ya miaka 3 kuanzia 2022 hadi mwaka 2025.


Mhandisi Mahona Luhende kutoka Tanroads makao makuu amesema kuwa jingo la abiria linatarajiwa kuwa na maeneo ya abiria wa ndani, abiria wan je pamoja na abiria maalum ambapo linatarajiwa kuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.2 kwa mwaka.

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram