65 views 15 secs 0 comments

FIMBO AWATAKA WANANCHI KUACHA KUTUMIA DAWA KIHOLELA BILA KUFATA MAELEKEZO NA USHAURI

In KITAIFA
July 12, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Mamlaka ya Dawa na vifaa tiba TMDA imewataka watanzania kuacha kutumia dawa kiholela bila kufuata maelekezo na ushauri wa wataalamu badala yake amesisitiza matumizi sahihi ya dawa Ili kupunguza tatizo la usugu wa maradhi.

Hayo Ameyasema Leo 9 julai 2024 mkurugenzi mkuu wa TMDA Adam Fimbo Amesema Katika maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea Katika viwanja vya mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam

Dkt Fimbo Amesema Mamlaka hiyo inaendelea kupambana na usugu wa vimelea vya dawa na kuelimisha jamii Katika kuhakikisha dawa zinatumika Kwa ufasaha na usahihi Kwa kufuata maelekezo sahihi ya kitaalam.

“Usugu wa dawa umekuwa ukiongezeka siku Hadi siku kutokana na matumizi ambayo sio sahihi na kupelekea wananchi wengi kupata madhara” Amesema Dkt Fimbo

Aidha Amesema TMDA imeshiriki maonesho ya sabasaba mwaka huu Ili kutoa elimu Kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya dawa na kufahamu majukumu ya Taasisi hiyo.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram