Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme EDTCO imejipanga kuhakikisha inakamilisha miradi mbalimbali ya Usambazaji Umeme Nchini inakamilika katika kipindi Cha mwaka wa fedha 2024, 2025.
Ameyabainisha hayo Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi EDTCO Dismas Masawe mara baada ya kukutana Waandishi wa Habari Katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es salaam ambapo amesema Moja kati ya Mradi unatekelezwa ni Mkoa wa Katavi Wenye thamani ya shilingi Bilioni 116 ambapo unaotarajiwa kukamilika mwaka huu.
Masawe amesema tayari wameshaunganisha Umeme zaidi ya vijiji 130 vilivyopo Mkoani Mbeya Mradi ambapo unegharimu zaidi ya Bilioni 50 ambapo Wanatarajia kumalizia kusambaza Umeme Vijiji 30.
Kwa Upande wake Meneja wa Fedha EDTCO CPA Mnyembi amesema Kila mwaka kiwawango Cha fedha kinaongezeka katika Kampuni hi hivyo mwaka huu 2024 Wanatarajia kupata zaidi ya shilingi Bilioni 90.