Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Kampuni ya Usimamizi wa mitaji Sanlam investment inayofanya kazi katika Nchi 25 za Afrika Mashariki imeanza rasmi kufanya kazi nchini Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya CRDB ikilenga kutoa fursa kwa Taasisi,Vikindi na mtu mmoja mmoja kuwekeza kupitia mfuko maalum wa Sanlam pesa Money Market Fund unaotoa faida ya gawio kulingana na mtaji.
Hayo Ameyasema Leo 08 Julai 2024 wakati wa Uzinduzi wa Sanlam investment jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa mamlaka ya usimamizi wa Masoko na Usalama wa Mitaji Nicodemus Mkama ametoa wito kwa watanzania kutumia Fursa ya kuwekeza kupitia mfuko Sanlam Pesa money utakao wawezesha kukuza mitaji na kupata mikopo itakayo wawezesha kupiga hatua za Maendeleo
Mkama amesema Mfuko huo utaiwezesha Serikali kupata fedha pindi Wananchi watakapo jitokeza kuwekeza na fedha ambazo zitasaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo hapa Nchini.
“Tutahakikisha Kampuni yetu ya Sanlam inashirikiana vizuri na Serikali na kuleta Maendeleo kwani Mfuko huu umekidhi vigezo katika kukuza bidhaa zake Kwa Umma,” amesema Mkama.
Ameongeza kuwa Sanlam inatoa fursa kwa watu wenye mitaji midogo kukuza mitaji yao kwa kuwekeza kuanzisha shilingi elfu 10 ambapo gawio watakalo pata litapelekea mitaji kukua na kujikuta wakitimiza Malengo waliyo jiwekea na kukuza uchumi wa Familia.
Nae Mwenyekiti wa Sanlam East Afrika Julius Magabe amesema Sera yao inahakikisha huduma zao zinatolewa katika Taasisi, Makampuni, Watu binafsi na Vikundi ambapo lengo ni kuleta Mapinduzi katika Uwekezaji hapa Nchini
“Huduma hizi tunazileta zitasaidia Jamii na kuwezesha Wananchi kupata Gawio ambapo Soko la Tanzania linatoa fursa wezeshi za Kiuchumi hivyo tumefungua milango ya kuwafikia Watanzania kuanza kuwekeza Kwa kiwango cha chini kuanzia shilingi elfu kumi ya Kitanzania,” amesema Magabe.