73 views 48 secs 0 comments

DCI KINGAI AKABIDHI VYETI VYA HESHIMA NA ZAWADI KWA ASKARI WALIOFANYA KAZI VIZURI ZAIDI DAR ES SALAAM

In KITAIFA
July 09, 2024

Na Mwandishi wetu WAMACHINGA
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini Kamishna wa Polisi Ramadhani Kingai leo Julai 9, 2024 Katika ukumbi wa Maofisa wa Polisi uliopo Oystabey Kinondoni amewakabidhi vyeti vya heshima askari 13 wa Jeshi la Polisi waliofanya kazi vizuri zaidi kwa mwaka 2023/2024

CP. Kingai amesema askari hao wamepewa vyeti na zawadi hizo kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Jeshi la Polisi (Police General Orders) na Kauli mbiu ya Jeshi la Polisiย  ya Nidhamu, Haki weledi na uadilifu.

“Nimewatunuku vyetu askari 13 wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ambao hawa wachache wanawakilisha wenzao, askari wanaofanya vizuri ni wengi ambao ni wazuri pia.” Alisema CP Kingai

“Vyeti na zawadi hizi zinalengo laย  kuwapa motisha na morali askari wengine kujituma zaidi ili nawao watambulike” CP Kingai aliongezea.

Katika hatua nyingine CP . Kingai amesema kuwa hali ya usalama nchini imeimarika kutokana utendaji mzuri wa askari kama hawa waliopewa vyeti.

Kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Denis Simbeye kwa niaba ya waliopewa zawadi ameshukuruย  kwa kutambuliwa mchango wao na kuahidi kuwa ataendelea kuimarisha nidhamu ya utendaji kazi na cheti alichopewa kitakuwa hamasa hata kwa askari wengine ili waweze kufanya vizuri zaidi.

Zoezi hili la kuwatambua askari waliofanya vizuri zaidi hufanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu jumla ya askari 13 wametambuliwa na kupewa vyeti na zawadi.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram