74 views 2 mins 0 comments

RC CHALAMILA AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI AHAMASISHA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

In KITAIFA
July 06, 2024



-Asema Katika uchaguzi huo, watakaochaguliwa ni Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa pamoja na Wajumbe Watano [5]

-Ataja sifa muhimu za Mwananchi kujiandikisha na kushiriki uchaguzi huo

-Abainisha uhakiki wa Maeneo ya Kiutawala

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 06,2024 amekutana na waandishi wa habari ofisi kwake Ilala Boma kwa lengo la kuhamasisha wakazi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

RC chalamila amesema uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 wanaochaguliwa ni Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa pamoja na Wajumbe Watano [5] wanaounda Kamati ya Mtaa ambapo wapiga kura ni Wakazi walioko katika mitaa husika.

Aidha RC Chalamila alitaja sifa za mwananchi kujiandikisha kushiriki uchaguzi huo ni pamoja na awe Raia wa Tanzania, awe na Umri wa miaka 18 au Zaidi, awe ni mkazi wa eneo la Kitongoji au Mtaa husika ,asiwe na ugonjwa wa akili uliothibitishwa na Daktari anayetambulika na Serikali au Bodi ya Utabibu na awe amejiandikisha kupiga kura katika Kitongoji au Mtaa husika.

Sanajari na hilo RC Chalamila alibainisha Kuhusu Uhakiki wa Maeneo ya Kiutawala ambapo amesema OR-TAMISEMI imeshafanya uhakiki wa maeneo ya kiutawala na  Mkoa wa Dar es Salaam umebakia na maeneo yake ya awali yanayojumuisha Wilaya 5, Tarafa 12, Kata 102 na Mitaa 564. Hivyo uchgauzi huu wa Serikali za Mitaa Utafanyika katika Mitaa yote 564. Mgawanyo wa mitaa hiyo nika ufuatavyo;- Wilaya ya Ilala Mitaa 159 , Kinondoni Mitaa 106, Temeke Mitaa 142, Kigamboni Mitaa 67, Ubungo Mitaa 90

Mwisho RC Chalamila ametoa rai kwa wananchi kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kuwa wapiga kura katika tarehe na vituo vitakavyoelekezwa pia kuhakiki majina na taarifa zao katika vituo vya kupigia kura katika tarehe na siku zitakazokuwa zimeelekezwa

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram