80 views 44 secs 0 comments

BODI YA SUKARI YATOA MSIMAMO WA SERIKALI

In BIASHARA, KITAIFA
July 05, 2024

Na Mwandishi wetu WAMACHINGA

BODI ya Sukari nchini Tanzania imesema msimamo wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwalinda wananchi, wakulima, wawekezaji na wadau wengine muhimu kwa kuhakikisha inafanya maboresho makubwa kwa maslahi ya Watanzanaia wote.

Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania Profesa Kenneth Bengesi, aliwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya kupitishwa sheria mpya ya sukari nchini.

โ€œTunaendeleza majadiliano na wadau ili kutatua changamoto zote sambamba na kuikuza sekta ya sukari kwa sababu ni jambo nyeti na muhimu, hivyo tunalichukulia hili kwa umakini,โ€Alisema Profesa Bengesi.

Kwa siku za karibuni kumekuwa na mijadala kadhaa kutokana na siku chache zilizopita kugubikwa na uhaba wa sukari hali iliyoibua hofu kwa Watanzania wote.

“Tangu tulivyo binafsisha hadi sasa uzalishaji bado haujatosheleza mahitaji ya nchi, hivyo pengo la uzalishaji bado lipo na mfumo uliokuwa ukitumika miaka ya nyuma kuingiza sukari ya kuziba pengo tulikuwa tukitumia wafanyabiashara, lakini  kwa sababu ilionekana kwamba sukari iliyokuwa ikiingia nchini ilikuwa ni kiasi kikubwa ambacho kilikuwa kikivuruga utulivu wa soko la ndani. Ilipofika mwaka 2015 serikali ilichukua jukumu la kufanya mabadiliko ya kanuni za sheria ya sukari za mwaka 2010 na kubadilisha mfumo wa uingizaji wa sukari” Prof.   Kenneth Bengesi, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram