Na Mwandishi wetu WAMACHINGA
Azitaka taasisi za dini kushirikisha Serikali kusimamia maadili
Wizara ya Maendeleo ya Jamii Shirikisheni wadau
Azitaka taasisi za umma na Serikali kuwa mfano bora kwenye jamii kuhusu maadili
Asisitiza maadili kupewa kipaumbele katika Mtaala wa Elimu
Serikali itaendelea kusimamia na kukuza uadilifu wa maadili kama msingi wa maendeleo endelevu kupitia Sera na Sheria bora kwa kushirikisha wadau wa kidini, elimu, na jamii ili kuendeleza utamaduni ambapo maadili yatajumuishwa katika kila sehemu ya maisha ya Watanzania.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko katika uzinduzi wa Kitabu kiitwacho “MMONYOKO WA MAADILI NANI ALAUMIWE”, ambacho kimeandaliwa na kuandikwa na Mhe. Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally Mbwana, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Julai 3, 2024 BAKWATA Makao Makuu jijini Dar es Salaam.