230 views 32 secs 0 comments

DMI WAANDAA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA TATU JIJINI DAR ES SALAAM

In KITAIFA
June 27, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Chuo Cha Bahari Dar es salaam DMI Kwa kushirikiana na chuo Cha Bahari Cha Ghana wameandaa kongamano la Tatu ambalo linalotarajia kufanyika Julai 4 na 5 Katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es salaam

Ameyasema hayo Leo Tarehe 27 Juni 2024 Mkuu wa chuo Cha Bahari Dar es salaam DMI Dkt Tumaini Gurumo Amesema kongamano hilo la kimataifa linatarajiwa kujumuisha nchi 11 ambazo ni Kenya,Komoro,Liberia,Ghana, Nigeria,Sieraleone,Demark,Italy,Sweeden,Korea kusini na china

Gurumo Amesema Moja ya kazi mama ya Taasisi ya DMI ni kuandaa makongamano ya kitaaluma yenye lengo la Kujenga uelewa Kwa jamii Kuhusu faida ya sekta ya Bahari



Aidha Gurumo Amesema kongamano hili ni la Tatu kwani kongamano la kwanza lilifanyika mwaka 2022 na la pili lilifanyika mwaka 2023

“Kongamano hili la Tatu linatarajiwa kufunguliwa na Naibu waziri mkuu na waziri wa Nishati Mhe.Dkt Dotto Biteko tarehe 4 Julai kuanzia Saa tatu kamili asubuhi”.Amesema Gurumo

Kauli mbiu ya kongamano hilo ni-“KUIENDEA KESHO: KUJUMUISHA ULINZI NA USALAMA WA MAJINI, MABADILIKO YA TABIA YA NCHI NA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA KWA UKUAJI WA UCHUMI WA BULUU”

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram