269 views 25 secs 0 comments

RC MAKONDA ABAINISHA JUMLA YA WANANCHI 6434 WAHUDUMIWA KWA SIKU 2

In KITAIFA
June 26, 2024

Na Mwandishi wetu WAMACHINGA ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda, amebainisha kuwa tangu kuanzia kwa kambi ya madaktari bingwa na wabobezi mkoani humo siku ya tarehe 24 Juni, 2024 na hadi kufikia jana tarehe 25 Juni, 2024 tayari jumla ya watu 6434 wamehudumiwa vema na kupatiwa na kusema kulingana na takwimu za siku hizo mbili zimebainisha ongezeko la watu kwa kila siku hali inayowapa mwanga wa kusudio la kuongeza dawa zaidi pamoja na madaktari.

“Juni 24, 2024 tulihudumia watu 2034, Juni 25, 2024 tulihudumia watu 4400 hivyo kufanya jumla ya watu 6434 kuwa tayari wamehudumiwa kwa muda wa siku mbili maana yake inatutaka sisi kuhakikisha tunaongeza dawa kwasababu hatutaki mwananchi yoyote aondoke hapa bila kupata dawa na tutaongexa vifaa zaidi vya maabara pamoja ma kuongeza madaktari na mabanda zaidi, niwaambie nimeshaongea na RMO tunatafuta mabanda mengine na madaktari wengine kuongexa kasi ya huduma”

RC Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na maelfu ya wananchi waliojitokeza kupatiwa huduma katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid katika kambi ya madaktari bingwa na wabobezi aliyoianda kwa kushirikiana na wadau wengine mbalimbali.


#KambiYaMadaktariBingwaNaWabobezi
#ArushaYaSamia
#KaziIendelee

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram