83 views 3 mins 0 comments

WAZIRI MAJALIWA AZINDUA RIPOTI ZA KIDEMOGRAFIA, KIJAMII, KIUCHUMI NA MAZINGIRA ZINAZOTOKANA NA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA 2022

In KITAIFA
June 23, 2024

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa (Mb) amezindua rasmi Ripoti za Kidemografia, Kijamii, Kiuchumi na Mazingira zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi na Sensa ya Majengo ya Mwaka 2022.

Amezindua ripoti hizo leo Juni 22, 2024 katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo umewakutanisha wadau mbalimbali na viongozi akiwemo, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa.

“Ni siku muhimu kwa kuwa leo tutashuhudia uzinduzi wa ripoti za Kidemografia, Kijamii, Kiuchumi na Mazingira zilizotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 Chapisho namba nne.

“Pamoja na ripoti ya kina iliyotokana na taarifa zilizokusanywa katika Sensa ya Majengo Nchini mwaka 2022.

Waziri Mkuu amesema, ripoti inayohusu majengo yote ni ya kwanza kutolewa nchini tangu kuasisiwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Akizungumzia kuhusu umuhimu wa matokeo ya taarifa zilizokusanywa katika sensa zote tatu mwaka 2022, Waziri Mkuu amebainisha kuwa,

“Matokeo haya ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa letu kutokana na matumizi yake. Hii ni kutokana na ukweli kwamba ripoti za matokeo ya Sensa zitakazozinduliwa hivi punde zinatupa fursa muhimu kama nchi kuendelea kutambua kwa kina zaidi hali zetu kidemografia, kiuchumi, kijamii na mazingira pamoja na hali ya makazi.”

Pia, amefafanua kuwa, baadhi ya matokeo muhimu katika ripoti za takwimu za msingi zimedhihirisha matokeo chanya ya utekelezaji wa mipango ya kimkakati inayofanywa na Serikali zote mbili katika sekta mbalimbali.

“Matokeo yameonesha kuwa tumepiga hatua kubwa katika sekta ya elimu. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, kiwango cha kujua kusoma na kuandika kwa watu wenye umri wa miaka 15 na kuendelea kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kimeongezeka hadi asilimia 83.0 mwaka 2022 kutoka asilimia 78.1 ilivyokuwa mwaka 2012.

“Kwa upande wa sekta ya nishati, matumizi ya nishati safi kwa ajili ya kupikia yameongezeka hapa nchini ambapo, kaya zinazotumia umeme kwa ajili ya kupikia zimeongezeka kutoka asilimia 1.6 mwaka 2012 hadi asilimia 4.3 mwaka 2022 na Gesi kutoka asilimia 0.9 mwaka 2012 hadi asilimia 9.4 mwaka 2022.”

Amesema, idadi ya kaya zinazotumia kuni aiili va kunikia zimepungua kutoka asilimia 68.5 Haya ni mafanikio makubwa katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira. Sote tunafahamu kuhusu madhara yanayosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa ambayo ni pamoja na kuchangia ongezeko la athari zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, athari kwa afya za watumiaji pamoja na kuleta athari nyingine za kiuchumi katika jamii.”

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram