176 views 4 mins 0 comments

RAS NGUVILA AZINDUA KAMPENI YA “AFYA CHECK” 2024 KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM

In KITAIFA
June 21, 2024

Na Mwandishi wetu WAMACHINGA DAR ES SALAAM

-Ataja umuhimu wa kampeni hii kwa wananchi wa Dsm

-Asema Madaktari Bingwa na Wabobezi katika taalum mbalimbali ni sehemu ya kampeni hiyo na  ataja huduma zitakazotolewa

-Aainisha Ratiba ya Upimaji Afya katika ngazi za Wilaya zote

-Awashukuru wadau wote waliowezesha kampeni hiyo


-Kwa upande wake Dr. Mohamedi Mang’una amewaasa wananchi kupima Afya zao kupitia kampeni hii ili kupatiwa Ushauri na Matibabu sahihi kwa wakati

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar Es Salaam Dkt. Toba A. Nguvila Leo tarehe 20 Juni, 2024 amezindua kampeni ya Siku kumi ya  “Afya Check” 2024 yenye Upimaji Bure wa Afya  kwa Wakazi wa Wilaya zote tano za  Mkoa wa Dar es Salaam katika Viwanja vya Barafu – Mburahati -Ubungo.


Dkt. Nguvila ametaja umuhimu wa kampeni hiyo kuwa ni Kuwapa Wakazi wa Dar es Salaam fursa ya kupima Afya zao hasa Magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza sambamba na kuwajengea wananchi Hamasa na Utamaduni wa kupina Afya zao kila wakati

RAS Nguvila amesema kuwa huduma zitakazotolewa ni kuanzia ngazi ya Afya ya Msingi Hadi huduma za Kibingwa na kibobezi ambapo madaktari hao watakuwa ni sehemu ya Kampeni hii Aidha, huduma zitakazotolewa ni pamoja na
Uchunguzi na Matibabu ya Magonjwa ya Akili, Uchunguzi wa Saratani za aina mbalimbali, Uchunguzi wa Magonjwa ya Macho, Uchunguzi wa Afya ya kinywa na Meno, Uchunguzi wa Magonjwa ya Moyo, Uchunguzi wa Shinikizo la damu, Uchunguzi wa Magonjwa ya kina Mama na Watoto, Uchunguzi wa Ugonjwa wa Kisukari, Uchangiaji wa Damu kwa Hiari, Chanjo kwa Watoto chini ya miaka 5 na Magonjwa mengine ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza



Hata hivyo, Dkt. Nguvila ameainisha ratiba ya upimaji wa Afya katika ngazi za Wilaya zote kama ifuatavyo

-Manispaa ya Ubungo tarehe 20-21 Juni, 2024 katika Viwanja vya Barafu – Mburahati
-Manispaa ya Kinondoni tarehe 22 -23 Juni, 2024 Viwanja vya Biafra
-Jiji la Dar es Salaam
tarehe 24 -25 Viwanja vya Mnazi Mmoja
-Manispaa ya Temeke
tarehe 26- 27 Viwanja vya Zakhem- Mbagala
-Manispaa ya Kigamboni
tarehe 28-29, Juni 2024 Viwanja vya Mji Mwema



Dkt. Nguvila aliwashukuru Wadau wote waliowezesha kampeni hiyo kufanyika wakiwemo MDH, FHI 360, AMREF, CRDB  JHPIEGO, WORLD VISION, Jumuiya ya Mabohora, MNH,  MOI, JKCI, ORCI AMANA, MWANANYAMALA, TEMEKE, na Hospitali zote 5  za Wilaya,  AFYACHECK, MSD,  JHPIEGO, Damu Salama na Hospitali Binafsi za Kairuki, JK, Agarwals dental, Smiles Dental na Ndovu Clinic  kwani mchango wao unaenda kufanya Afya za Wakazi wa Dar es Salaam kuwa Bora sambamba na kuwakumbusha wazazi na walezi kuwapeleka Watoto chini ya miaka mitano kupata chanjo



Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Dr. Mohamedi Mang’una amesema kutokana na ongezeko kubwa la Magonjwa pamoja na vifo vinavyosababishwa na Magonjwa yasiyoambukiza ni vema wananchi kupina Afya zao kupitia kampeni hii na baadae kupatiwa Ushauri na Matibabu sahihi kwa wakati



Ikumbukwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya Uwekezaji Mkubwa katika Sekta ya Afya ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam ikihusisha Miradi ya Maendeleo, Ununuzi wa Vifaa Tiba vya kisasa,  Ajira ya Watumishi wa Afya na kusomesha wataalam katika fani mbalimbali katika nyanja za ubingwa na ubingwa bobezi hii imepelekea Nchi yetu kuwa kitovu Cha Tiba ya Utalii (medical tourism) katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati



*”PIMA AFYA YAKO KWA UMUHIMU WA KESHO YAKO”*

/ Published posts: 1212

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram