71 views 2 mins 0 comments

TCRA WANAJIIMARISHA KUFUATILIA VYOMBO VYA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI WANAOPOTOSHA HABARI

In KITAIFA
June 14, 2024

Na Mwandishi wetu WAMACHINGA DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imesema inajiimarisha kufatilia vyombo vya habari na waandishi wa habari wanaopotosha habari hususani katika kipindi cha kuelekea uchanguzi wa serikali za mtaa na uchaguzi mkuu wa nchi kwani waandishi wengi wanaonekana kuwa na tatizo la kusoma namba hali inayopelekea kuandika takwimu zisizo sahii.



Haya yamesema na Muwakilishi wa TCRA  Andrew Kisaka katika warsha ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na tumehuru ya uchaguzi jijini Dar es salaam,ambapo amesema waandishi wa habari wanapaswa kutumia taaluma vizuri na kuzingatia maadili ya uandishi wa habari na sio kuandika vyovyote ili tu kuvuta wasomaji na kupata watazamaji wengi bila kuangalia athali ya kile wanachokiandika.



“Waandishi wa habari mnatakiwa msome,kama mtu anaipenda hii kazi basi atalazimika kusoma ili kuwa na uelewa ni ngumu sana kwa muandishi kuelimisha umma wakati we mwenyewe hauna kitu kichwani,Media ni kama kisu ukikitumia vibaya kinaleta athari,sasa tunapoelekea katika uchaguzi 2024 /2025 tumejipanga kufatili ili kupata habari zilizo sahihi sio zenye kupotosha kwa lengo la kuvutia biashara ya kupata idadi kubwa ya watazamaji”Amesema Andrew.

“Hakuna serikali yoyote iliyo na nia ya kuzima mtandao kwa sababu zisizo Julikana,tusione kwamba ni kipaumbele cha serikali kuzima mtandao hakuna hiyo lakini tuelewe kwamba media ni kama kisu,ukiitumia vibaya madhara yake ni makubwa mno”Amesema Andrew kisaka Meneja wa huduma za utangazaji na mhandisi wa maswala ya mahusiano ya TCRA wakati akijibu swali liliouliza ni kwanini TCRA huzima huduma ya mtandao katika kipindi cha matokeo ya uchaguzi mkuu? Katika warsha ya siku mbili ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na Tume huru ya uchaguzi.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram