111 views 2 mins 0 comments

TRC WAZINDUA SAFARI YA DAR-MORO KUANZA SIKU YA IJUMAA

In KITAIFA
June 12, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

***Treni ya SGR haijaja kuchukua nafasi ya ndege Wala Mabasi

****Mizigo mikubwa haitakiwi,chakula Wala Wanyama inaitaji kuwa Treni ya kimataifa

Shirika la Reli Tanzania TRC limezindua Safari ya Treni ya Mwendokasi kutoka Dar es salaam Mpaka Morogoro Na kuanza Rasmi safari hiyo siku ya ijumaa ya Tarehe 14 Juni 2024

Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja kadogosa Ameyasema hayo Leo Tarehe 12 Juni 2024 wakati akizindua Kampeni hiyo ya Safari ya DAR-MORO Amesema Katika kutimiza agizo la Mhe.Rais shirika linataarifu umma kuanza kutoa huduma za awali za usafiri wa Treni wenye viwango vya kimataifa vya SGR DAR-MORO



Amesema kuanza Kwa safari ya Abiria ya Dar es salaam_Morogoro ni sehemu ya Kuendelea kujifunza  Kwa kuwa Teknolojia mpya nchini na kijilizisha Kwa mifumo mbalimbali ya uendeshaji wa huduma za usafiri wa Treni kabla ya kuanza Rasmi safari ya kutoka Dar mpaka Dodoma ifikapo tarehe 25 julai 2024

“Uendeshaji ambao unaoanza baada ya shirika kijilizisha uendeshaji wa miundombinu,Vitendea Kazi Kwa maana ya vichwa na Mabehewa Kwa lengo la kujifunza matakwa ya kisheria kuhakikisha Vitendea Kazi Njia na mifumo ya mawasiliano inafanyiwa majaribio kabla ya uendeshaji Ili kuhakikisha usalama wa Abiria”Amesema Kadogosa



Kadogosa Amesema Abiria wanaweza kukata tiketi kwa njia ya mtandao au madirisha ya kukatia tiketi ndani ya Steshen Kupitia njia ya mitandao unaweza kukata Siku Moja,Siku Tatu Mpaka wiki kabla ya safari kuanza na kutokana na msongamano wa Steshen

Kadogosa Amesema kuhakikisha kutunza miundombinu ya treni mpya ya Mwendokasi SGR na Ile Treni ya zamani wameeka sheria kuwa Uruhusiwi kuingia na chakula,mizigo mikubwa,wanyama,Nk



Aidha kadogosa Amesema SGR haijaja kuchukua nafasi ya RELI ya zamani,Ndege Wala Mabasi Bali Amesema Kwa uharaka wa safari yako unaweza kutumia SGR kutokana na muda

Kwa upande wa Mkurugenzi wa TCB BANK Adam Mhayo Amesema Katika mradi huu wa kimkakati TCB bank imeshirikiana na TRC Katika maeneo kadhaa Katika kutoa huduma ya malipo na kufanikisha kuleta vichwa vya Treni na Mabehewa kutoka Ujerumani



“Tumeingia makubaliano na shirika la Reli Tanzania Ile huduma ya malipo mteja anapoenda kukata tiketi kwa Ile platform mzima itakuwa karibu na Tcb bank”Amesema Mhayo

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram