Na Mwandishi wetu WAMACHINGA
TAASISI ya Mama Ongea na Mwanao kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wametoa msaada wa Baiskeli 250 kwa watoto wenye mahitaji maalumu (Walemavu) ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao za kupata elimu .
Akizungumza na Waandishi wahabari leo Juni 11, 2024 jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Steve Nyerere amesema baadhi ya wazazi wamekuwa wakipitia wakati mgumu mara baada ya kujifungua watoto wa aina hiyo kwani wanaume huwatelekeza wake zao.
“Kuna wanaume ni wazembe katika kulea Watoto wenye Ulemavu hufikia kuwa kana kuwa mtoto mwenye Ulemavu si wake, lakini mtoto akiwa na hana ulemavu anamdai mwanamke kuwa mtoto ni wake,” amesema Nyerere.
Nyerere meongeza kuwa hali ya mtoto mwenye uhitaji haimzuii mtoto huyo kupata Elimu.
Amebainisha kuwa Kupata Mtoto Uhitaji ni Mipango ya Mungu nasio Mikosi na kuitaka jamii kuondoka na Dhana hiyo.
“Sisi tunahitaji kupeleka Mahitaji kwa Wenye uhitaji popote walipo hivyo tunaomba taasisi nyingine zituunge mkono,” amesisitiza Steve Nyerere.
Kwa upande wake Katibu wa Taasisi Ongea na mwanao Evon Sherry amesema taasisi hiyo imetembelea mikoa mitano na kubakisha mikoa miwili kwa jili ya Viti mwendo kwa wahitaji.
Amesema kampeni ya “Baskeli yaShule ya Mama” inalenga kumsaidia mtoto mwenye uhitaji kupata Elimu.
“RaisDk.Samia Suluhu Hassan anawasaidia wakina mama katika sekta ya Afya,Maji lakini Sisi tumeamua kumtua mama mtoto mgongoni” amesema Evon.