Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Katika kuhakikisha burudani hazipoi na kuwafikia watanzania Hatushikiki imekuja na kuzama kwa jua ili kukuza sekta ya burudani na kuwafanya wasanii kutoa burudani ya aina yake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendajiย wa Kalito’s Way Group of Companies, Carlos Kalito, amesema kuwa wana sheherekea mafanikio ya biashara yake ya migahawa nchini Tanzania yatokanayo na ubunifu kwa kutoa nafasi kwa wasanii mbalimbali

.
Kampuni hiyo, ambayo inajumuisha migahawa ya Samaki Samaki, Kuku Kuku, na maarufu Wavuvi Kempu, inaajiri jumla ya Watanzania 500 kwa kuweza kutoa burudani za usiku.
“Maadhimisho ya miaka 17, yaliyopewa jina la “Hatushkiki Tunaua Kila Siku,” Kalito alisisitiza mazingira mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania kama sababu kuu ya mafanikio yao.

“Nina fahari kuchangia soko ajira kwa wasanii mbalimbali kutoa burudani licha ya changamoto, hasa ushindani wa soko. Tuna watu wabunifu na wavumbuzi ambao wametusaidia kufikia mafanikio haya, na tunaendelea kusonga mbele.