Na mwandishi wetu WAMACHINGA
-Akagua maendeleo ya barabara ya Tabata Mazda hadi Kimanga
Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 10 ,2024 amefanya ziara ya kushtukiza kukagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mazda kimanga Km 3.7 Wilaya ya Ilala.
RC Chalamila amefanya ukaguzi huo kufuatia ahadi aliyoitoa kwa wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wa kuongea na wananchi wa eneo hilo alioufanya Tabata Kimanga Mei 30,2024.
Mhe Albert Chalamila amemtaka mkandarasi anayejenga barabara hiyo kuongeza kasi ili mradi ukamilike kwa wakati, wananchi wa maeneo hayo waweze kuitumia katika shughuli zao za kila siku za kujiletea kipato.
Aidha RC Chalamila amesema Rais Dkt Samia ameelekeza nguvu kubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali hapa nchini hususani Mkoa huu, โNiwatake makandarasi waliobahatika kupata kazi kufanya kazi kwa welediย kuzingatia muda na thamani ya
pesa โ Alisema RC Chalamila
Vilevile RC Chalamila ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuelimishana juu ya kutoziba mifereji ya maji taka pia kutotupa taka ovyo ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa kuziba mifumo ya maji taka
Sanjari na hilo RC Chalamila amewataka wananchiย kutokuwa na shaka kuhusu kusua kusua kwa ujenzi wa barabara hiyo ambapo amesema atakuwa anafuatilia kwa karibu maendeleo ya barabara hiyo pale atakapoona kuna shida atachukua hatua stahiki mara mmoja
Mwisho RC Chalamila ametoa rai kwa wananchi kuendelea kulinda amani ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa ndicho kitovu cha uchumi wa nchi, Diplomasia na mambo mengine mengi yenye maslahi mapana kwa nut mmoja mmoja, Taifa la Tanzania, na mataifa mengine Duniani