103 views 14 secs 0 comments

TANZANIA INA UMEME WA KUTOSHA KUFANYA SHUGHULI ZA KIUCHUMI-DKT BITEKO

In KITAIFA
June 09, 2024



Asisitiza hakuna mgawo wa umeme*

Amshukuru Rais Samia kuiimarisha Sekta ya Nishati*

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, kwa sasa nchi ina umeme wa kutosha  kuwawezesha Watanzania kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Juni 9, 2024 wakati alipoungana na Waumini wa Kanisa la AIC Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita kwenye ibada ya jumapili.

“Nashukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia ameweka mipango madhubuti kwenye sekta yetu ya nishati ambayo sasa imepelekea tuwe na umeme wa kutosha na hatuna mgawo wa umeme.” Amesema Dkt. Biteko

Ameongeza kuwa,  miezi michache iliyopita, tatizo la mgawo wa umeme  lilikuwa likimkosesha amani, lakini  kwa juhudi za viongozi Wakuu wa Serikali, Wizara na TANESCO limefikia tamati.

Kutokana na uwepo wa umeme mwingi wa  kutosha, Dkt. Biteko amewataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo na kwamba Serikali inaendelea kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram