
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
JUMUIYA ya wafanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es salaam, wametoa rai kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA kutumia njia ya ushirikishaji katika kukusanya mapato, badala ya kutumia njia zisizofuata misingi ya kisheria ikiwemo vishoka.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Juni 07/2024 Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashira Kariakoo Martini Mbwana Amesema kuwa katika kikao kilichoongozwa na Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu kijaji aliwaahidi wafanyabiashara kuongeza bajeti ya wizara kwaajili ya kuboresha mazingira ya biashara,kuwakutanisha na TRA na kuweza kuangalia namna ya kupunguza utitiri wa kodi.
” Tumewaomba TRA wanapotekeleza majukumu yao wasijifiche,tushirikisha e ,tufanyekazi kwa pamoja tujenge nchi yetu sote, wafanyabiashira tupo tayari kulipa kodi bila shuruti, Nipende kutoa wito kwa TRA hata wanapoleta vijana wapya katika kukusanyakodi watutambulishe wasinifiche wakawa wanawawinda wafanyabiashara”.Amesema Mbwana
Aidha Mbwana Amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa kipaumbele kikubwa kwa wafanyabiashara ambapo wamekutana na wizara zaidi ya tano ikiwemo wizara ya fedha na wizara mama ya viwanda na biashara na kufanya mazungumzo yanayochangia uboreshaji wa mazingira ya biashara nchini.
Aidha amebainisha baadhi ya Kero zinazoendelea kuwakabili wafanyabiashara hao kuwa ni pamoja na VAT,namna ya uwasilishaji wa risiti za EFD, na uingizaji wa mizigo kutoka nje.
Wafanyabiashara wanaomba kodi zote ziishie bandarini na si kuwafwata mara kwa mara katika maeneo yao ya biashara ili kuepusha mianya ya rushwa.
Aidha Jumuiya hiyo ya wafanyabiashara wa Kariakoo wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara kuwapa kipaumbele wafanyabiashara wazawa katika mradi wa uwekezaji wa soko la kimataifa la Ubungo,Wamesema wanahofu kubwa kwamba soko la Ubungo huenda lika athili biashara ya soko la kariakoo iwapo hakuta undwa sheria za kulinda wafanyabiashara wazawa.
Mbwana amesema wanaiomba serikali kuwa 70% ya maduka yamilikiwe na wazawa kwani wakija wageni wakamiliki hilo soko wataathili wafanyabiashara wazawa”wakija wachina wakaleta biashara zao na mzawa akasafiri kwenda China akaleta bidhaa ileile,mchina atauza kwa bei ileile ya China kwa vile anakiwanda huyu mfanyabiashara mzawa lazima atakosa namna ya kuuza hiyo inaleta hofu kwamba biashara zetu zitakufa,tutakosa ajira”Amesema Mbwana