Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila Amesema Jiji la Ilala pamoja na Halmashauri za Manispaa ya mkoa wa Dar es salaam Ni marufuku Kuendelea Kujenga ujenzi wa kutawanyika Kwa sababu ya Ardhi yake haipo kama ya mikoa mingine
Hayo ameyasema Leo Tarehe 30 Mei 2024 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila Amesema ujenzi huu wa ghorofa ndo ujenzi unaotegemewa kuonekana Katika Jiji la dar es salaam, Wilaya na Halmashauri zingine za mkoa wa Dar es salaam
“Ukiona majenzi mengine yakijengwa itakuwa ni ushamba mkubwa sana kwenu nyinyi watoto wangu kama mukiondoka hapa na division 4 au division 0 Kwa majengo haya,musome Kwa bidii,muwe na nidhamu,muwena heshima na Nia ya kuweza kufanya vizuri Katika mitihani yenu”. Amesema Chalamila
Shule ya sekondari ya minazi mirefu iliyojengwa Kwa gorofa ambayo imegharimu Kwa kiasi ya shilingi Bilioni 1 na milioni 700 iliyopo Katika maeneo ya gongolamboto,Kipawa
Pia Chalamila Amesema Serikali imeandaa mikakati Kwa kila Mwalimu wa shule za sekondari kuvaa sare za kitambaa Cha suti Katika Jiji la mkoa wa Dar es salaam
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila Amesema wameandaa baadhi ya uniform za walimu ambazo zitakazotumika Katika mikutano Mbalimbali
Amesema baada ya kitambaa hicho itakuja na pesa ya shilingi elfu 80 cash Kwa kila Mwalimu Elfu 50 itakuwa Kwa ajili ya kiatu na elfu 30 Kwa ajili ya mashono
Nae Mkuu wa shule ya sekondari Minazi mirefu Mwalimu Avalini chuguru Amesema Anashukuru serikali Kwa kuwajengea jengo la gorofa lenye madarasa 20 na matundu 45 ya vyoo pamoja na lifti Kwa wanafunzi wao.
MIUNDOMBINU YA KUBOMOLEWA HOSPITAL YA MUHIMBILI
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa Serikali inakusudia kuibomoa Hospitali ya Taifa Muhimbili karibu yote na kuijenga upya, kwa si chini ya Bilioni mia tano na sitini hivi karibuni.
“Hiyo itafanyika kwa ushirikiano wa Tanzania chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Korea, Hivyo safari hizi za Mheshimiwa Rais ni kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania” amesema Chalamila
Ameyasema hayo leo katika wilaya ya Ilala, alipotembelea zahanati ya kinyerezi, jijini Dar es Salaam kuangalia huduma zinazoendelea katika zahanati hiyo, ambao ni mradi wa Serikali kwa ajili ya kusaidia wananchi wa eneo hilo.