77 views 2 mins 0 comments

BARABARA ZA VIWANDANI KIWARANI KUKARABATIWA

In KITAIFA
May 30, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila Akiendelea na ziara yake ya siku tatu na Leo ikiwa ni siku ya kuhitimisha ziara yake Katika Wilaya ya Ilala na kuendelea kusikiliza kero za wananchi.

MKUU wa mkoa Amekitembelea kiwanda cha nondo kiitwacho Metro Steel kilichopo katika Halmashauri ya Magharibi ya  Dar es Salaam;  kwa ajili ya kujionea uzalishaji wa nondo,pamoja na kusikiliza changamoto zilizopo kwenye kiwanda hicho ambapo kilio chao kikubwa ni barabara inayopelekea  kushindwa kusafirisha nondo hizo kwa wateja.

Amesema wawekezaji kama hawa ambao wapo Katika hatua ya kwanza mara nyingi huwa wanasumbuka sana,huwa tunatanguliza maslahi,bila ya kuangalia maslahi mapana baada ya kuazishwa Kwa kiwanda

“nchi nyingi ambapo utakapo kwenda kunakuwa na maeneo yaliyoandaliwa Kwa ajili ya uwekezaji ambayo yako savey,wanajanza umeme,njia za maji na kwenye ramani nzuri,na hata hizi barabara ambazo wateja wetu wanazilalamikia Kwa faida ya uwekezaji wa kiwanda hichi sisi kama serikali tunawajibu mkubwa wa kuhakikisha barabara hizi zinatengenezwa”Amesema Chalamila

Kwa upande Mwingine Chalamila ametoa Rai kwa viongozi wote wa Serikali, kwamba ni muda wa kurahisisha na kusaidia biashara ambayo inawasaidia wawekezaji kuweza kuchangia maendeleo ya mfumo wa biashara zetu hapa nchini.

” Kukiwa na kiongozi yoyote ambaye anaweza akakwamisha hili, maana yake wafabiashara na wawekezaji wanaweza wakashindwa kufanya biashara , na kiwanda hiki kikifungwa maana yake tutakua tumefunga ajira ya watu wengi sana, kuliko hata pato la kawaida la Taifa” amesema Chalamila



Pia amewapongeza wawekezaji wa kiwanda cha Metro steel lakini pia amewasihi kukumbuka kurudisha huduma kwa jamii.



Aidha  Muhandisi wa TARURA Ilala, Reginald Mashanda amesema wameshaandaa mikakati ya kuweza kutekeleza  utengenezaji wa barabara kwenye bajeti inayoanza mwezi wa saba, lakini pia kwa vile eneo la viwanda lina mahitaji makubwa ambapo kuna magari makubwa ya kubeba mzigo, kwahiyo TARURA imeanza usanifu wa barabara zote za viwandani ili ziweze kujengwa kwa kiwango kizuri na pia kwa sasa, jambo la dharura katika barabara hii ya Kiwalani zitapita Greda kwaajili ya kusawazisha barabara.

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram