89 views 2 mins 0 comments

TRA AWATAKA WAANDISHI WA HABARI ZA MTANDAONI KUWAHAMASISHA WANANCHI KUTUMIA DESTURI YA KUDAI RISITI

In BIASHARA, KITAIFA
May 29, 2024

Na Mwandishi wetu WAMACHINGA

Mamlaka ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imewaomba waandishi wa habari za Mtandaoni (digital online) kuhamasisha wananchi kuwa na desturi ya kudai risiti pale wanapofanya manunuzi ili kusaidia kuwapata wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi.



Rai hiyo ameitoa leo Jijini Dae es salaam Mei 29,2024 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mapato TRA Elimu ya elimu ya mlipa kodi na Mawasiliano kwa Umma Hudson Kamoga katika Semina ya kwanza na Jukwaa la  Waandishi wa habari wa Mtandaoni (JUMIKITA) ambapo amesema waandishi hawana budi kuwa wazalendo na taifa lao kuweza kumsaidia Mhe Rais kwa kuwaelimisha wananchi kudai risiti pale wanapofanya manunuzi kwani kodi   ni fedha inayosaidia miradi mbalimbali ikiwemo   Barabara, hospitali,shule



“Tunatambua kuwa dunia imekuwa kijiji kwa ajili ya Mitandao ya kijamii hivyo kundi hili la waandishi wa habari wa mtandao watatusaidia sanaa kwani kuna wafanyabiashara wengi wanafanyabishara kidigital kupitia semina hii italeta tija kwa Wananchi kukusanya mapato  huko walipo na kuwajengea utamaduni wa kulipa kodi kidigitali bila usumbufu wowote” amesema Kamoga

Hata hivyo amesema kuna utaratibu wa kukusanya kodi kwa njia ya mtandao kwani wamegundua kuna baadhi ya wafanyabishara hawana ukaazi Tanzania lakini shughuli zao hutumia hutumia mitandao ya kijamii kukutana na wateja wao  hivyo kupitia wanahari wa mitandao watasaidia kuwafikishia elimu ya namna ya kulipa kodi .


Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la  Wanaandishi wa  habari Mtandaoni JUMIKITA Shabani Matwebe ameshukuru sanaa TRA kutambua mchango wa wanahabari wa mtandaoni kwa kuwapatia semina adhimu kwa mara ya kwanza hivyo italeta tija kuongezeka kwa mapato kwani wale wanaotumia simu janja wataipata elimu huko huko walipo.

/ Published posts: 1212

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram