258 views 43 secs 0 comments

SAMIA KUPITIA NCHIMBI AKAMILISHA.AHADI MRADI WA UCHUMI MANYONI

In KITAIFA
May 29, 2024

Na Mwandishi wetu WAMACHINGA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk Samia Suluhu Hassan leo kupitia Katibu Mkuu wa chama hicho Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi amekipatia chama wilaya ya Manyoni zaidi ya shilingi millioni 18 kwa ajili ya kuezeka jengo lake la kitega uchumi.

Katibu Mkuu wa CCM alitangaza hayo mbele ya Kamati ya Siasa ya Wilaya, mjini Manyoni, mwanzoni mwa ziara yake ya siku mbili mkoani Singida.

Amesema hiyo ilikuwa ni ahadi ya Mwenyekiti Rais Samia aliyoitoa kupitia kwa Katibu Mkuu wa zamani Daniel Chongolo.

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram