70 views 2 mins 0 comments

RC CHALAMILA AWAPA ONYO BALOZI WA CANADA NA PSSSF NDANI YA WIKI MOJA

In KITAIFA
May 29, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila Atoa agizo kwa wale ambao walionganisha mfumo wa Maji taka kwenye mifumo ya maji safi PSSSF na Balozi wa Canada wakabomoe wenyewe ndani ya wiki Moja

Ameyasema hayo Leo Tarehe 29 Mei 2024 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila Amesema wasipofanya hivyo atachukua jukumu Kwa haraka sana amesema atakamata wakurugenzi wake na kuwashughulikia Kwa utaratibu



“Nitakamata wakurugenzi na kuwashughulikia Kwa utaratibu na hata Balozi wa Canada aambiwe haraka sana Ili waweze kusafisha mji kinyume na hapo watashitakiwa Kwa sababu wamekusudia kuuwa watanzania Kwa kusababisha magonjwa ya kulipuka

Chalamila amepiga marufuku Kwa wale wanaoosha Magali pembezoni mwa barabara Amesema swala hili lisichukuliwe kisiasa



“Na Wala sitaki mwanasiasa yoyote alizungumzie hili,huwezi kuweka pamvet alfu pembeni umeeka dumu la elfu Moja”Amesema Chalamila

Amemtaka mkurugenzi wa Ilala kama Kuna maeneo ya biashara wapangishe Kwa wale wanaoosha Magali atangaze kwenye mfumo watu wakaombe



Mkuu wa Wilaya ya ilala Edward Mpogolo Amesema Jiji la dar es salaam tumejipanga kukomesha changamoto ya Kujaa Kwa maji mara nyingi ya mvua ambayo inayotokana na changamoto ya mifereji Kwa mda mrefu.

Katika maeneo ambayo yanachangamoto ni A Plaza,CBE,kamata,na maeneo ya Muhimbili, maeneo hayo yote huwa yanajaa maji



“Leo hii tunakuonesha tumejipanga Jiji la dar es salaam limejipanga Kwa ajili ya kutokomeza changamoto hiyo

Aidha Mkuu wa Wilaya Amebainisha kuwa Kuna baadhi ya watu waliojenga majengo makubwa wanachapisha maji machafu kwenye mifereji ya maji safi na taasisi zengine

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram