Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ALBERT CHALAMILA ameziagiza mamlaka za Usimamizi wa maji safi DAWASA, DART pamoja na TARURA kuboresha miundombinu ya maji taka pamoja na ujenzi ujenzi wa barabara katika mtaa wa lindi kata ya gerezani wilaya ilala jijini Dar es salaam
Ameyasema hayo Leo Tarehe 29 Mei 2024 mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila katika ziara maalumu ya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika jiji la Dar es salaam
Ziara hiyo ya kusikiliza kero za wananchi inamfikisha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ALBERT CHALAMILA katika mtaa wa lindi kata gerezani jijini dsm kushuhudia changamoto za miundombinu ya barabara pamoja na mitalo ya kupitisha maji taka
Ambapo anasema changamoto hiyo natokana na ujenzi mbovu wa miundombinu hiyo Kutokana na uzembe wa usimamizi wa ujenzi wa miundombinu hiyo mkuu wa mkoa anatoa agizo kwa wasimamizi hao
Chalamila Anaenda mbali zaidi na kuziagiza balozi mbalimbali nchini pamoja jengo la PSSF lililoko posta jijini DSM kuondoa mifumo ya kupitisha maji taka katika njia za maji safi.
Ubovu wa miundombinu ya barabara, ujenzi holela wa makazi pamoja na ujenzi mbovu wa mitalo ya kupitisha maji taka unatajwa kuwa ni wimbo wa taifa ambapo kwa kiasi kikubwa maeneo mengi nchini kukumbwa na mafuriko