112 views 2 mins 0 comments

RC CHALAMILA APANDA HELKOPTA KUANGALIA MAENEO AMBAYO YALIYOPATA ATHARI ZA MVUA JIJINI DAR ES SALAAM

In KITAIFA
May 28, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila Amesema mkoa wa Dar es salaam umeharibika Kwa miundombinu ya mvua nyingi ambazo zilizoweza kunyesha na kuathiri Kwa ujumla miundombinu ya nchi

Ameyasema hayo Leo Tarehe 28 Mei 2024 Katika viwanja vya ndege Terminal 1 Ambapo Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila Amepanda ndege ndogo na viongozi wengine Kwa ajili ya kuangalia athari zilizotokea katika Mvua zilizonyesha Jijini Dar es salaam hivi karibuni


Chalamila Amesema maeneo ya Target Moja ni maeneo ambayo ni karibu na bonde au mito kuangalia athari za mvua kwenye bonde la mto msimbazi,Mto mlalakua,Mto Tegeta na Mto nyakasangwe na Mto Mpiji

“Kuna baadhi ya maeneo maji yametuama sana Sasa maji Yale yanaweza sababisha mambo makubwa mawili,Moja ni kuaribu miundombinu na la pili ni  kuweza kusababisha magonjwa”Amesema Chalamila



Aidha Amebainisha kuwa wapo na wataalamu wa maji wa kuangalia namna Gani jinsi ya kushauriana Ili kusaidiana Ili maji yaweze kutoka baadhi ya maeneo “angalau wananchi wetu Kwa Sasa Katika kipindi hichi Mvua zimetulia tumepata majawabu ya kutosha”Amebainisha Chalamila

“Mhe Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ameendelea kutoa fedha Kwa ajili ya kurudisha miundombinu ambayo imekwisha athirika na maswala kadhaa”Ameongeza Chalamila



Pia Chalamila Amesema wapo na wataalamu wa Ardhi ambao wataruka na ndege hiyo Kwa ajili ya kuangalia Kwa namna Gani Kwa kwata zinaathiri mkwamo WA maji kuelekea yanapotaka kwenda alfu waje na majawabu ya pamoja Ili kuona nini kinaweza kufanya kusaidia wananchi wa mkoa wa Dar es salaam



Aidha Chalamila Amesema baada ya ziara hii Mainjinia wezi wao, Tarura,Tanroads,Dawasa pamoja na RMO Watakaa Kwa pamoja Ili waaze Kwa haraka sana kazi ya kurudisha miundombinu na kutengeneza mifereji pale ambapo wananchi wao wanaweza kupata athari Kwa hasa Kwa mvua za mwaka unaofata

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram