
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbarawa Amewataka watanzania kujitokeza Kwa wingi kupanda treni ya Mwendokasi hasa wale wa Daraja la Tatu,ambayo Treni hiyo imeangaziwa vigezo vyote vya nauli
Hayo ameyasema Leo Tarehe 24 Mei 2024 wakati wa ziara yake aliyoifanya Jijini Dar es salaam Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbarawa Amesema Treni hiyo Itaanza Rasmi Tarehe 14 Kutoka Dar es salaam Mpaka morogoro na anaamini Tutaeka Bei ambayo itawavutia watanzania wengi

“Sasa hivi Kuna mchakato wa kupata Bei ambayo inasimamiwa na latra na wanalifanyia kazi,naamini itakuwa Bei nzuri,Bei ambayo itawezesha watanzania ,”
“Kuna baadhi ya watanzania wakisikia spidi 160,tunaitaji wapate frusa na wao waje angalau wakisikia spidi 160 waone jinsi kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia suluhu”Amesema Mbalawa

Aidha Amesema vivuko vyote vinatalajiwa kumalizika kabla ya tarehe 14 Juni mwaka huu Ili magari yaweze kupita juu ya vivuko na tarehe 10 ndo mwisho wa kumaliza vivuko Kwa ajili ya kupitisha treni ya abiria ya Dar es salaam mpaka morogoro
Ameongeza kuwa Treni ya Dodoma itaanza rasmi Julai 25 kwani Bado inafanyiwa majaribio mpaka kufikia mwezi julai itakuwa imeshakamilika

Kwa Niaba ya Mkurugenzi mkuu wa Trc Masanja kadogosa Amesema kipande Cha Dar es salaam, Morogoro kipo Asilimia 97.69,Katika vipande vya morogoro Makatopora kipo Asilimia 96.73 pia vipande vya Makatopora Tabora kipo Asilimia 14.34 na Tabora isaka ipo Asilimia 5.8 na isaka mwanza Asilimia 57.08
Kadogosa Amesema utekelezaji wa Tabora Hadi kigoma Bado unaendelea kipande Cha sita kipo Asilimia 5.49 na utaratibu wa manunuzi unaendelea Kwa RELI ya uviza msongani
