Na Mwandishi wetu ZANZIBAR WAMACHINGA
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar Bi. Safia Iddi Muhammad amefanya uteuzi wa wagombea kutoka vyama 14 vya siasa kuwania nafasi ya Ubunge katika Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika tarehe 8 Juni, 2024.
Ameyasema hayo Leo Tarehe 23 Mei 2024 Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la kwahani,WILAYA ya mjini mkoa wa mjini magharibi, Zanzibar Sadia iddi Muhammad Amesema amefanya uteuzi huo leo ikiwa ni siku ya uteuzi baada ya wagombea 14 waliochukua fomu za uteuzi kurejesha fomu hizo na kukidhi masharti ya kuteuliwa kugombea Ubunge katika jimbo hilo.
Safia Amesema Wagombea walioteliwa na vyama vyao kwenye mabano ni Bi. Nuru Abdalla Shamte (DP), Bw. Bashir Yatabu Said (Demokrasia Makini), Bi. Mwanakombo Hamadi Hassan (NLD), Zainabu Maulid Abdalla (CCK), Bi. Tatu Omary Mungi (UPDP), na Bw. Khamis Yussuf Mussa (CCM).
Aidha Amebainisha kuwa Wengine walioteuliwa ni Bi. Jarade Ased Khamis (AAFP), Bw. Kombo Ali Juma (NRA) Bi. Shara Amran Khamis (ADC), Bi. Naima Salum Hamad (UDP), Bi. Madina Mwalim Hamad (ADA-TADEA), Bw. Amour Haji Ali (SAU), Bi. Mashavu Alawi Haji (UMD) na Bw. Abdi Khamis Ramadhan (CUF).
“Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi huo mdogo, wagombea hao wanatarajia kuanza kampeni za uchaguzi kuanzia tarehe 24 Mei, 2024 hadi tarehe 7 Juni, 2024 na siku ya uchaguzi ni tarehe 8 Juni, 2024″Amesema Safia