167 views 3 mins 0 comments

WANANCHI KUJENGEWA KUJUA UMUHIMU WA KUTUMIA MAZIWA KATIKA WIKI YA MAZIWA

In BIASHARA, KITAIFA
May 22, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Wizara ya Mifugo na Uvuvi Kupitia Bodi ya maziwa inaelekea Katika kuazimisha wiki ya Maziwa ambayo itakayofanyika Tarehe 1 Juni 2024 yenye kulenga utumiaji wa maziwa Kwa kila mwananchi na kupewa ufahamu wa jinsi ya utumiaji Kwa maziwa yote ambayo yaliyosindikwa na yasiyosindikwa.

Msajili wa Bodi ya maziwa Prof George Mutani Msalya Amesema siku hiyo ya wiki ya Maziwa ni kutoa elimu ya maziwa na Tasnia ya maziwa Kwa ujumla umuhimu wa maziwa na mchango wake Kwa lishe,uchumi na ajira Katika nchi yetu ya Tanzania.



Hayo ameyasema Leo Tarehe 21 Mei 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari Katika washa iliyofanyika Katika wizara ya Mifugo na Uvuvi juu ya kuelimisha kutoa elimu ya maziwa

Msalya Amesema wapo watu wengi ambao Bado wanatoa habari mbalimbali za upotoshaji kuhusiana na maziwa muhimu kusema kuwa mfano, maziwa ya watoto pekee ikiwemo kwamba maziwa hayana umuhimu Katika uchumi.



“Hali yetu ya Tasnia nchi ikiwemo hali ya uzalishaji tumeona hapa kwamba tnazalisha maziwa Lita Milioni 3.9 nchi nzima licha ya kuwa na ng’ombe wengi sana, na Tanzania ni ya pili kuwa na Mifugo Katika Bara la Afrika lakini mifugo yetu mingi inazalisha maziwa kidogo kidogo”Amesema Msalya

Aidha Amebainisha kuwa uhitaji wa maziwa yetu nchini ni Lita Milioni 12 Kwa mwaka na kunaupungufu wa Lita Bilioni 9 iliiweze kujitosheleza Katika maziwa,na tunakuwa tunaagiza kiasi Cha kutosha Cha maziwa kutoka nje ya nchi



“Mwaka Jana 2023 tuliagiza Lita Milioni 11 kutoka nchi Zaidi ya kumi na tunatumia shilingi Bilioni 23 na unaona tunatumia pesa nyingi sana kuagiza maziwa nchi za nje,kumbe hii ni fursa ambayo tungeweza kuitumia tungeweza kuokoa pesa zetu nyingi ambazo zingeenda Katika mahospitali kuliko kuzitumia na kwenda kununulia maziwa”Ameongeza Msalya

Nae Joseph Mabula Mratibu wa Mradi wa TI3P Amesema B milad Foundation ilitupatia Dola milioni 7 za kutusaidia Ili ziweze kutusaidia kuweka mazingira wezeshi Kwa ajili ya wafugaji wa Tanzania Ili waweze kupata mikopo ambapo bank ya maendeleo ya kilimo imetenga Dola milioni 40 Kwa ajili ya kuwekeza Katika sekta ndogo ya maziwa



“Katika mradi huu unalenga Zaidi kuwanufaisha Hawa wafugaji wadogo wadogo lakini ni Kwa Kujenga haya Mahusiano kati ya wale wasindikaji na wakulima wadogo wadogo ambao ndo wazalishaji wa maziwa”Amesema Mabula

Msalya Ameongeza kuwa Mradi huu unatekelezwa Katika mikoa 15 ambayo ni mikoa ya nyanda za juu kusini na nyanda za juu kaskazini mikoa ya Tanga,Dar es salaam na PWANI na pamoja na Kanda wa ziwa na kule Zanzibar Katika mradi huu tunashirikiana na wezetu ambao ni wataalamu wa sekta ya Mifugo ambao wanatusaidia Katika nyanda za juu, kaskazini pamoja na mikoa hiyo

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram