81 views 25 secs 0 comments

DC MPOGOLO AFUNGUA UMISSETA WILAYA YA ILALA

In KITAIFA, MICHEZO
May 22, 2024

Na Mwandishi wetu Wamachinga


Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mkoani Dar es salaam, Edward Mpogolo, amefungua mashindano ya Umoja wa Shule za Sekondari-UMISSETA Wilaya ya llala

Mashindano hayo yameshirikisha wanafunzi kutoka Majimbo ya Ilala, Segerea na Ukonga kwa ajili kuunda timu ya Wilaya Ilala.

Watakaochaguliwa wataunda timu ya kanda itakayokwenda ngazi ya Mkoa wa Dar es salaam.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Ilala,ย  Mpogolo, amefungua mashindano hayo katika viwanja vya Shule ya Sekondari Pugu.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya, amesema Michezo ni sera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)katika Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ambayo ni kujenga afya na mahusiano katika jamii.

โ€œLeo tunazindua mashindano haya ya Wilaya Ilala nawaomba vijana wangu mkafanye vizuri katika timu ya Kanda muwe na maadili mazuri kambini na nidhamu bora kuleta ushindi katika wilaya yenu kwa kuchukua vikimbr vyote โ€œamesema.

Mpogolo amesema ofisi yake kwa kushirikianana Meya wa Halmashauri ya jiji na Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam,watakuwa karibu na Kambi ya Wachezaji wa Ilala mpaka watakapokwenda kushiriki UMISSETA Taifa.

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram